Wakenya wengi wanaona ufahamu wa Kiingereza kama kipimo cha akili au ustaarabu. Lakini huku Tanzania, mambo ni tofauti. Huku, Kiingereza hakimaanishi chochote cha kifahari — kwa kweli, mara nyingi ni lugha ya walevi na “wasanii wa mitaani.” ![]()
Kwa Mtanzania wa kawaida, Kiswahili ni kila kitu — kuanzia serikalini hadi vyuoni. Ukiongea Kiingereza kupita kiasi, watu wanaweza kukuona kama unaringa au huna mzizi wa nyumbani. Tanzania ni nchi pekee Afrika Mashariki ambako Kiswahili kimepewa hadhi ya juu kitaifa.
Kwa mfano, bunge la Tanzania linaendeshwa kwa Kiswahili. Sheria zinaandikwa kwa Kiswahili. Hata hotuba za Rais – Kiswahili. Lakini Kenya? Waheshimiwa wanang’ang’ania Kiingereza mpaka wengine wanafumua grammar live kwenye TV. ![]()
Wakati Wakenya wanajitahidi kuonesha umahiri wao kwa lugha ya mkoloni, Watanzania wanaitumia Kiingereza tu pale panapobidi – mara nyingi ni kwenye kazi rasmi, au pale ambapo Kiswahili hakiwezi kufikisha ujumbe vizuri.
Sasa, mtu akija na Kiingereza barabarani Dar es Salaam – kuna uwezekano mkubwa atadhaniwa ni mlevi, msanii, au anatafuta kiki. Kwa nini? Kwa sababu watu wa kawaida hawana muda wa kutafuta impression — wanachapa kazi kwa lugha wanayoelewa kwa undani: Kiswahili.
Wakenya wanasema: “Mbona Watanzania hawajui Kingereza?”
Jibu ni rahisi: Wanajua, lakini hawajali.
Kiswahili kinawatosha kufanya maendeleo, kujadili sera, na hata kufundisha masomo ya chuo kikuu.
Je, hii inamaanisha Wakenya wako juu kwa sababu wanazungumza Kiingereza vizuri zaidi?
Siyo lazima. Lugha ni chombo, siyo kipimo cha akili. Mtu anaweza kujua Kiingereza kizuri lakini asiwe na hoja yoyote ya maana. Tanzania imewekeza kwenye utambulisho wa lugha ya taifa.