It was a day like today, Christmas day eve when I was arrested in tao na makarao. Together with a couple of maboys we decided kuenda reggae Hollywood club. So kushuka tao tukaenda kuchukua mbachu pale karibu tea room, kutoka kwa vaite tunakanyaga mdogo mdogo tukielekea Mokhtar dada street.
Tunakaribia City market sahio ni kama saa tano usiku hivi tunasikia tunduru tudogo tudogo. Kucheki ma pink handle kadha ndo hao wanakata kijiko kuelekea biashara street bado wakipiga huto tunduru twao. Hatuku wa mind so tukaendelea kutembea saizo tumejijaz ki @Jirani style.
Kidogo tunasikia fala fulani gizani akituita akisema “nyinyi majamaa simameni hapo”. Tukaendelea tu kutembea, mwingine akarudia tukamsho ajipatie shughuli. What we did not know was that they were plain clothed police on patrol.
Nikasho maboy hawa wanakaa makarao, na kwa hio story tutoke teke. Maboy kuzuba zuba mimi huyo nikatoka mbio, maboy kuona hivyo nao nyuma yangu. Makarao wakaanza kupiga firimbi wakisema simama ama tufyatue. Nilijiambia hio risasi wacha inipate na huko mbele. Na yenyewe kitu waliona ni kisogo na rubber ya sole ikipiga ile kona ya kujoin Koinange street. Ilibidi watufuate mbio.
Kuingia Koinange street wale mapoko walikuwa wamejianika nao wakatoka teke sahizo hata hawajui kwa nini tunahepa. Mmoja wao akanishika mkono akaniambia kam tujifiche hii side, si nikamfuata. Tukaingia chuom fulani tukatulia. Kidogo poko ameanza kunidara na sahio matension zimejaa. Kidogo poko ananiambia akona bahati juu mteja amejileta, ashaanza kunipigia bei sahizo bado ananishikashika. Nikajiambia, haizuru sio kila siku kunaendaga hivi. Nikamsho tuende shot ya haraka juu bado lazima nipate maboy wangu tuingie reggae. Kumaliza hio shot nikasho huyo poko atulie nichek maboy ndo nirudi tumalize biashara.
Mimi kutokea tu kwa barabara side za Mokhtar dada hivi pa, nikapatana na hao makarao head on. Kumbe bado walikuwa wanapiga mwenda na maboy wangu wakitafuta ule boy mnono. Walikuwa sure nimepotelea tu mahali hapo. Maboy wangu nao walishikiwa kwa mlango ya club before waingie. Ma bouncer walikataa wasiingie juu ya kuogopa ngori ya gava. Nikadandiwa kimalamala hivyo tu. Wacha ni charazwe mambao na bado nko juu ya mbachu yangu imenasa mbaya. Kidogo na mimi nikavalishwa pingu yangu tukaanza kutembea kuenda central. Najaribu kuongea na karao tuelewane lakini bado wamenishikia machungu juu ya kazi ya kifala ile nilikuwa nimewafanyisha.
Sisi hao tukafikishwa central, weh! Ni kama kulikuwa na bash ya viboko, tulinyoroshwa hapo kishenzi. Tukatoa njumu side moja na kupigwa tero before kuingizwa cell. Hio siku tuliwacha mbachu kilo ka sita kwa OB na njugu, gee na karafu plus fegi packo kadhaa though juu ya kuchanganyikiwa niliingia na taksin yangu kwa cell. Kuingia hivi kwa hio corridor tukapata mzito wa cell, chokosh fulani hivi anajiita Onyi ndo kusema. Tulipata kakijana kamenyang’anywa kila kitu kamewachwa na ngodha pekee yake. Onyi alisoma design tuliingizwa hapo ndani ki-VIP ikabidi ajipatie shughuli.
Saa sita usiku hivi makarao wakakam roll call yao. Tumepangwa kwa ki.line hivi. Tunaanza kuulizwa maswali za kifala ati umeshikiwa nini, kidogo karao mmoja anasema akicheka ile kicheko cha saitan ati mimi najifanya naweza kukimbia na vyenye nko mnono. Karao mwingine akanisongea akanipiga mbao ati “na wewe mujamaa mnono kwa nini unakula miraa kwa police station?” Nikaambiwa nimeze hio taksin fasta fasta hata nikaletewa maji kwa chupa ya kuiteremsha.
Sazile bado nimeshangaa itakuwaje, chokosh fulani akapasuwa, nadhani aliona ile mshangao ilikuwa kwa face yangu ikambamba. That was my salvation. Karao akaniacha akakuta huyo chokosh nikapata chance ya kutupa hio packin yangu. Nilikuwa natoka central after 3 days kama Christmas imepita, cuzo wangu alipeana thao tano ndo hio ngori ikuwe deleted.