Kwanza kabisa niwasalimu wanajukwaa, habari za muda huu. Natumai mu wazima, mimi pia nina siha njema. Shukrani kwake Jalali kwa kutujalia pumzi njema.
Kitu kilichonisukuma, kikanihimiza, kikanihamasisha hadi nikaweza kufungua uzi huu ni hii tabia ambayo nimeishuhudia kwa baadhi ya mabinti haswaa niliyokutana nao njiani kwenye safari za hapa na pale. Kwakweli nashindwa kuwaelewa, kiasi cha kufikia kuwatafsiri ni wenye matatizo kwenye sehemu kadhaa za bongo zao.
Mmojawapo nilikutana naye nikitoka jijini Dar kuelekea Moro, ndani ya basi la BM. Huyu alinikuta tayari nishaketi kitini, simu ipo mkononi naperuzi.
Ukaaji wake wa nguvu kitini, ukanifanya nimtazame. Tukagongana macho, nikampa salamu maana si vyema kuketi pamoja safarini pasipo walau kusalimiana. Mrembo akanijibu kwa uchangamfu, kisha ‘nikala boksi’ maana huwa si mwongeaji sana haswa kwa mtu nisiye na mazoea naye. Basi safari ikaanza, kufika kibamba tu. Kafungua mkoba wake katoa korosho za kuchomwa na juisi ya chupa. Kanikaribisha, bila hiyana nikashukuru ila si kukaribia. ‘Nikamlia bati tena’ nikawa naperuzi mtandaoni. Haijafika mbali kaanza uchangamfu na kuongea, nikaamua nimuunge mkono asijihisi vibaya. Ndipo nikajua mdada huyu ni mota ya kuongea, nikawa naenda naye sawa. Haujapita muda kaomba simu yangu, kaandika namba zake akasave na kujibip. Nikabaki nashangaa tu, akahamia kwenye SMS napo ni hivyohivyo.
Mwishowe akalala, nikashukuru nami nikajiegesha maana nilishachoka anahama mada hii na nyingine kama mwimbaji anayebadili ‘Melody’ kuendana na ‘beat’.
Basi alipoamka si akadaka simu yake, kuendelea ‘kuchat’. Nikafanya kosa la kutumia uchangamfu, yaani anajieleza mno hata mengine hakuulizwa.
Basi Alhamdulillah tukafika Msamvu, bibie akachomoka garini kama vile gari la wagonjwa linawahi mahututi kwenye ajali. Mimi nikawa sijali sana nikashuka, kisha nikamtumia ujumbe ‘kwaheri’. Maana hakuaga ikabidi niage tu, nguvu kubwa aliyoitumia garini kunizoea isingekuwa viziri
Afanalek! Naulizwa kwani ninataka nini, mara kujuana kwenye gari isiwe nongwa. Mara kila mtu si kamaliza safari yake, sasa wewe vipi.
Yaani SMS zikaongozana kama msafara wa JPM, nikajikuta nikicheka tu maana niliona nachat na mgonjwa wa akili.
JAMANI WANAJUKWAA AYA MBILI HIZO ZA MWISHO NDIYO DHUMUNI LA UZI HUU, NIWIENI RADHI KWA KUWACHOSHA NA MAELEZO MENGI. HIVI HUYU AKILI ZAKE ZIPO SAWA?
SI HUYU TU YUPO MWINGINE NILIKUTANA NAYE KWENYE MKUTANO WA JPM SUA, NAYE KATOA NAMBA HAKUOMBWA NA MBWEMBWE KIBAO. CHA AJABU ANAAGWA TU, ANALETA UJINGA.
WAPO NA WENGINE KADHAA NIMEAMUA NISIELEZE ILI NISIWACHOSHE.