few dating tips

[ATTACH]121815[/ATTACH]

  1. Hauwezi kumpenda mtu ambae binafsi hajipendi.

  2. Mtafute Mungu, fanya kazi kwa bidii then pata mwanamke/ mwanaume bora, ukifanya hayo mambo matatu kwa usahihi, suala la kufanikiwa litakuja lenyewe tu.

  3. Mwanaume aliye bora na mwanamke aliye mzuri hapimwi kwa idadi ya watu aliolala nao, ila kwa idadi ya watu aliopata ujasiri wa kuwaambia mimi tayari niko na mtu licha ya ushawishi mkubwa aliokumbana nao.

  4. Kuna aina ya wanawake ambao mwanaume kwa namna yoyote unahitaji kuwaepuka. Yule mwanamke anaedhani uzuri wake ni zaidi kuliko tabia yake.

  5. Heshimu hisia za mwenzako, usitumie kama silaha ya ku-compromise kupata kile unachokitaka. Hicho ndicho kinachotofautisha kati ya ‘wavulana’ na ‘wanaume’ na ‘wasichana’ na ‘wanawake’.

  6. Watu hatari katika mahusiano ni wale ambao huko mwanzo walidanganywa, walisalitiwa, na kuchezewa…

  7. Usimwite mwanamke kwamba yuko cheap kwa sababu amekua mrahisi kwako. Inawezekana kabisa amekua mrahisi kwako kwa sababu anakupenda, ila kwa wengine ni mgumu zaidi ya chuma cha pua.

  8. Wanaume na wanawake waliokamilika hawapo. Ila wanaume na wanawake bora wapo kila mahala.

  9. Kama unampenda mtu, mueleze ukweli ajue. Na kama humpendi pia mweleze ukweli. Tuko nyuma ya muda… Achana na Masuala ya kupotezeana muda…huo ni utoto.

  10. Ajabu ni kwamba, mwanamke/mwanaume anaweza kukusaliti. Mungu hawezi kukusaliti. Having God must be your primary focus then relationship should come second.

Weekend Njema…

10 Likes

oya safi sana hii kaka

Heko kwa kutuarifu tunayoyafahamu tayari

2 Likes

English version… Any volunteers to translate this foreign language

Too much Swahili. Summary pliz

Shukrani lakini…wayatekeleza haya mwenyewe ama watushawishi tu tuibadili mienendo yetu?

I like number 7