Fahamu kwa undani vito na madini yanayoendana na wewe

image

Maandiko ya kale yanadai Binadamu au mtu ametokana na minerals, yaani ametoka kwenye Mineral Kingdom au tuseme “mavumbini”. Ndio maana unasikia wataalam wanasema mtu fulani anapungukiwa madini ya chuma, au ya fedha au Carbon, Zinc mara madini ya Chuma nakadhalika. Mtu anatakiwa kula vinavyotoka ardhini moja kwa moja kwa sababu yeye ameunganishwa moja kwa moja na hivyo vitu. Sayansi ya Astrology inasema kila mawe na madini yaliyopo ardhini (gems & minerals) yana uhusiano wa moja kwa moja na kila mtu kutegemea asili ya Nyota yake. Unakuta madini au mawe fulani ya ASILI FULANI mfano Fire element yanashabihiana, huku ya Air Element yakishabihiana pia. Ndio maana kama wewe ni Nyota fulani, ukijua mawe na madini yanayoendana na nyota yako na jinsi ya kuyatumia na ukaanza kuyatumia, ni wazi kuna shari, maradhi na mambo kama hayo utayaepuka; na kuna nguvu chanya utavuna kwenye maisha yako zitakazokusaidia kwenye kazi zako na majukumu yako ya kila siku. Hii ni kwa sababu unachokiita wewe JIWE au CHUMA, kiroho ni mtu aliyelala kwenye hayo mawe/ madini. Kama anaendana na wewe, yaani ni nyota yako, ujue ‘umeula’ na kama haendani na wewe kinyota, ujue imekula kwako. Masonara uwa wanakutengenezea Pete yako KULINGANA na jiwe la Nyota yako. Ndio maana ni hatari sana kununua Pete mtaani. Kama ina madini yasiyoendana na nyota yako ujue hiyo Pete itakuwa sababu ya mateso yako, yawe kiafya, kiroho na au kiuchumi. Unaweza kununua Pete ukaivaa na kuanzia hapo mahusiano yako au ndoa yako ikavurugika au ukaanza kuugua maradhi ya ajabu ajabu au ukafukuzwa kazi, biashara zikaporomoka na nuksi za kila aina zikakuandama! Lakini wanaojua nguvu ya Vito vinavyosapoti nyota zao ndio wale unashangaa anaanza kuvaa Pete, ndani ya muda mfupi mambo yake yanamnyookea! Hii nayo ni siri mnayotakiwa kuijua. KUHUSU PETE. Kuna aina 5 za Pete: 1. Pete za urembo 2. Pete za bahati 3. Pete za majini 4. Pete za maagano (mikataba) 5. Pete za madaraka/ mamlaka USIVAE PETE BILA KUJUA SABABU YA PETE HIYO/ HIZO.

Kujua mambo mablimbali kuhusu elimu zinazohusiana na ulimwengu wa roho click here to visit our blog
tibazetutz.blogspot.com