EWURA mko wapi na wizi wa vipimo vya mafuta ktk masheli?

Habari zenu,
Huu wizi wakuibia wateja wa mafuta ktk haya masheli unakera. Jana nilienda kununua petrol lita 2 cha ajabu ktk chombo inasoma lita moja na nusu. Hii ishu nimeiona huku Geita live na ile sheli naihifadhi jina hata wateja wamepungua.
Sasa nawauliza EWURA wanafanya nn? Au ktk mafuta tunauziwa vapour pia?
Wajuzi mtujuze na Ewura muwatembelee hawa wenye masheli mara kwa mara.

Hawa Ewura inatakiwa wamulikwe sasa,walianza operation ya kukagua pump za mafuta pale Dar,wakafanya kama wiki 2 wameacha,wauzaji sasa wanajifanyia wanavyotaka kwa raha zao…

Inasikitisha sana… poleni sana…

Mambo mengi yanaendeshwa kiujanja janja…

Cc: @Mahondaw

Ukute wanakula nao…Ewura na WMA wote walewale tu.

Hii kitu ni kweli

Mwendo wa kupigwa tuuupu.

Shamba la Bwana Heri na Mbuzi wa Bwana Heri,yote yanakuwa heri mkuu.! Nafikiri umeelewa

Kazi yao kubwa ni kukusanya ile % kutoka kwenye bili zetu za umeme.

Aisee

Fuel station nyingi wana mtindo huo wa wizi