ELIMU YA TANZANIA IMEWEKWA "KWAPANI" MWA WASIOJITAMBUA.

Na Josephat K. Nyambeya.

Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako (PhD) jana bungeni kwa madaha na kwa kujiamini kabisa amekana kutumika kwa vitabu vya mtaala wa Elimu msingi unaoishia darasa la sita.

Amesema hakuna kitu kama hicho,lakini mbona huku mtaani ukiongea na baadhi ya walimu wanasema mtaala huo ulishaanza kutumika miaka mitatu iliyopita na tena naambiwa mpaka kuna walimu walipelekwa kwenye semina maalum ya kuhusu mtaala mpya unaoelekeza elimu ya msingi kuanzia 2020 nadhani itakuwa mwisho darasa la sita?

Na taarifa kutoka kwa walimu wanaofundisha shule za msingi wanasema mtihani wa darasa la nne wa mwaka huu umetungwa kwa muongozo wa mtaala huu wa elimu ya msingi ya kuishia darasa la sita.

Mwongozo huu wa kufanya elimu ya msingi iishie darasa la sita ulitolewa mwaka 2014 baada ya utafiti mrefu ulioongozwa na Maprofesa akiwemo Kitil Mkumbo ambae kwa sasa ni katibu mkuu wa wizara ya maji.

Profesa Ndalichako na naibu wake wameukana muongozo huu kwamba hawajawahi kuuona na haupo na hautumiki. My God these people are absent-minded. Watoto huko mashuleni wanajua watamaliza shule darasa la sita, walimu nao wanafundishia mitaala ya elimu ya kuishia darasa la sita, maafisa elimu nao wako kwenye mood ya kidarasa la sita. Waziri yupo Dar es Salaam anasema hatambui kitu kama hicho? Maana yake nini? Serikali haina coordination? Serikali imeukana muongozo wa elimu aliouacha Kikwete? Na kama wameukana kwa nini wasiwataarifu wananchi wote watambue ili watoto na wadogo zetu wasiendelee kupotoshwa na kulishwa matango pori.

Ndalichako ni msomi mzuri, natumai angekuja na jibu lenye hoja zaidi ya vijembe na kujikosha. Wabunge na wenyewe kwa kutambua mhimili wao ulivyokuwa na nguvu katika hatima ya taifa wallipaswa kufikiri zaidi ya kupiga makofi na kuomba kamati ya uchunguzi juu ya jambo hili ili kwa pamoja tuwe na jibu msingi juu ya hatima ya elimu ya Tanzania.

Hebu uchunguzi ufanyike kuujua ukweli wa hili na hebu waheshimiwa wabunge fanyeni utafiti jamani na muihoji serikali kama alivyofanya Mama Susan Lyimo leo maana hatujui tushike lipi.

Elimu yetu kwa miaka mingi imekuwa ikichezewa na hawa wasiojitambua namna watakavyo, hatuna msingi imara wa kusimamia katika elimu yetu. Kila mtu anafanya anavyojua, alipata kutokea Waziri mmoja chini ya utawala wa Ben Mkapa akaunganisha masomo ya Fizikia na Kemia kuwa somo moja, huu ulikuwa ni moja ya ujuha kuwahi kutokea nchini. Kemia na Fizikia ni masomo mawili tofauti kabisa lakini kwa kuwa ellimu yetu tumeiweka makwapani mwa wasiojitambua nao wanaipeleka watakavyo. Kitu kama hiki kisingefanyika bila baraka za baraza la mawaziri.

Kwa waliopata kusoma sekondari ya juu (Advanced Level Secondary Education) kwa michepuo ya PCM/PCB/PGM anajua jinsi wanavyohangaika kutumia vitabu vya vyuo vikuu vya nje, Tanzania haina vitabu vya kufundishia katika masomo ya Fizikia, Kemia na hata Hesabu wanafunzi wanatumia vitabu kama University Physics (UP) ambacho ni kitabu cha chuo kikuu huko nje na hata vipimo vyake (units) siyo za mitaala yetu, huko utakuta vitu vimewekwa kwa inches, yards, mile, pounds n.k huku sisi tunatumia sentimita, metres, kilomita, kg n.k …Kwa msingi huu unatarajia kuzalisha watu wa namna gani kama hauna muongozo wa kufundishia, wanafunzi wanajisomea somea tu kama mbuzi walioachiwa shambani. Cha zaidi unawafanya wawe watu wa kukariri, kuji overdoze na hata kujikatia tamaa, hawana muongozo, hawana mtaala unaojulikana na kutambulika.

Nikiwa kidato cha sita mwaka fulani shuleni kwetu walikuja wanafunzi wa chuo kikuu cha Huddersfield ch Uingereza sasa wakaja bwenini nilipokuwa mezani wakatukuta wanafunzi kibao tunajisomea, mimi nilikuwa nimeshika kitabu cha Roger Muncaster pembeni kipo cha Chand na mwingine anasoma University Physics, mwingine Nelkon walipovifungua vile vitabu na kuuliza topiki tunazozisoma katika mtaala mzima wa A-level kwa Physics walisema . You are confusing yourself. Hatukuwaelewa kwa mda ule maana wote hatukutambua jinsi tulivyokuwa na mzigo mzito wa kuuweka kwenye ubongo ila sasa nimetambua elimu inatu confuse sisi wenyewe. Hatujisomi.

Elimu yetu imekuwa ikizalisha watu wasiojiamini, wasioweza kusimama na kuwasilisha hoja, kutetea hoja au hata kushindana na wenzao, wananchi huko mitaani wanasikika wakisema wasomi wetu wanazidiwa na wa nchi za jirani, haya yote ni matokeo ya eliu yetu kuwekwa makwapani mwa wasiojitambua. Huu ni ukweli mchungu. Chezea vyote ila elimu usiiguse.

Kama nchi yetu itaendelea kwa mtindo huu wa kuchezea elimu yetu basi hatima yake ni kuzalisha VILAZA wengi waliopita madarasa kibao lakini hawana kipya kichwani. Tutakuwa tunazalisha watu wenye akili mgando na watu wa kushangilia shangilia tu, na tutaendelea kupangiwa na waliobahatika kuipata elimu bora yenye misingi bora.

Tusiendelee kumtafuta mchawi wa elimu huku tunamjua, tusiendelee kuwalaumu wahitmu wetu huku sote tunatambua akina Ndalichako ndio chanzo.

Rafiki yangu Natamani Kuiyona Tanzup kuanzia jana nimeyaamini maneno yako uliyoyaandika kuhusu Ndalichako mapema baada ya kuteuliwa kushika nafasi hii.

Ukiwa ccm uprofesor na PhD yako ni bure kabisa. Huwezi kutumia professional yako effectively. Zaidi utafanya anachohitaji bosi wako hata kama ni cha kipumbavu tena upumbavu uliokithiri. Kuna wakati huwa nawaonea huruma JK mrisho, na mawaziri wake hasa Shukuru Kawa-mbwa, na Membe