Dr. Leaky Abdallah, Mwl Kashasha Live TV1 wakichambua mchezo wa leo Kombe la Dunia

Shika remote yako, weka TV 1 kula uhondo, TBC wao bado hawajajiunga maana leo Bajeti inapitishwa hivyo wako bungeni Live, leo weka TV 1.

sawa

sisi wa azam tulishanyofolewa hii chanel.

Unaweza kuipata kwa kubadili mwelekeo wa dish lako, elekeza NYUZI 75E halafu TP 11596H30000 unaipata vzr kabisa TV1 na TV nyingine 38 za bongo na nje, kama huwezi tafuta fundi mwoneshe hii kitu atakusetia mitambo.

Unamaanisha kwa kutumia dish hili hili la azam?

Ndiyo, hata mimi natumia azam

[FONT=courier new]Sawa nimewaona jana ila nadhani Dk. Leakey is ’ outshining ’ Mwalimu Kashasha halafu ’ technically ’ kuwaweka hao Wawili kama ’ Soccer Analyst ’ haukuzingatiwa vizuri kwakuwa Wote wawili wana maeneo yao ’ bobezi ’ na nadhani Dk. Leakey angewekwa na ’ Mchambuzi ’ kama George Ambangile yule Kijana / Dogo wa Magic Fm au Jeff Leya wa Clouds Media Group au hata wangemuomba Msemaji wa Simba SC Haji Manara ambaye huko nyuma na bado anajulikana kuwa ni ’ Mchambuzi ’ mzuri sana wa mipira ingependeza sana na kutuvutia mno.

Mwalimu Kashasha katika Television hana ’ mvuto ’ halafu anaonekana bado ana hana data / details za kutosha hasa kuhusu Timu mbalimbali za Ulaya na mipira ya nje ya mipaka yetu ya Tanzania. Ukiondoa tu ’ umahiri ’ wake katika ’ Football Technical Jargon ’ Mwalimu Kashasha katika ’ Kuuchambua ’ mpira na kutuvutia Watazamaji wengi bado ana safari ndefu sana.

Kwa hili TBC1 na TV1 mmetukosea mno Wadau wenu. [/FONT]

Aisee nikweli Dk. Leakey ni level nyingine, mwalimu kashasha utasikia man to man marking, mara unajua football is possesing footwork square determination… Namaanisha wanakuwa wafanya square pass kwa kutumia middle fringes.

Kashasha mzuri VPL, FIFA bora hata Steve moyo Mchongi na Ballistic Missile (Baruan Muhuza)

Mashati yao ya vitenge kama wako kwenye mbio za mwenge

satellite ipi tuingie

Sipendi kuangalia kwa sababu Dk Leakey anapewa airtime ndogo, wakati ana madini ya kutosha.

Mwl kashasha yupo vizuri kwenye uchambuzi wakiufundi uwanjani.

Dk leakey yupo vizuri kwa historia tena ya kugoogle.