Nadhan tunafaham kuna aina nyingi za doughnuts lakini leo naomba niwajuze za kutengeneza simple za nyumbani
Mahitaji
Mafuta chupa moja na nusu
Unga wa ngano kg 2
Mayai 4
Maziwa fresh au mtindi pakt moja
Sukar robo
Bakin powder hapa sisemei zile simba mbili nasemea baking powder yenyewe sababu ukiweka zile simba mbili yanajiachia na kula mafuta kopimo cha baking powder n vijiko viwili na nusu vya chakula
Namna ya kutayarisha
Chukua mafuta nusu vunjia mayai humo kisha yapige yajichanganye na mafuta
Unga wako mimina sukari changanya sukar ichanganyike weka baking powder kama vipimo vinavyosema
Kwenye mchanganyiko wa mafuta mimina maziwa yako kwa mkupuo changanya pamoja kisha mimina kwenye unga wako
Changanya ukiona bado havichangamani mimina maji kidogo kidogo had unga wako ushikane na usiwe mlaini sana
Nafaham kuna vifaa na maalum vya kukatia shape ya doughnuts lakini kama huna uwezo tayarisha glass na chupa ya soda
Baada ya kuchanganya unga wako kata matonge makubwa hata matatu
Nyunyizia unga kwenye kibao cha chapat sukuma tonge lako lisiwe jembamba liwe zito sawazisha duara la tonge lako chukua glass chovyea kwenye unga wa ngano zungushia kwneye tonge ulilosukuma kutoa shape kisha chupa ya soda izungushe kati kati ya shape ole ulokatakutoa dot la kati kama hivi hapa chini[ATTACH=full]178695[/ATTACH]kisha tayarisha karai mafuta yale chupa moja mimina yapate moto hakikisha ukilitumbukiza mafuta hayawi moto sana yatababua