Hawayuuni wanakijiji.
Muriegaini; mbiyoreini; idhinade-ini; mulembe-ini; chamgei-ini; na kadhalikaini. Hayawi hayawi, mwishowe yamekuwa. Kwa wale ambao wako na dual-citizenship, ama ukipenda wanakijiji wenzetu ambao wako katika hii dayaspora, ni kuwaarifu tu kwamba tunarudi hewani hapo kesho saa moja alfajr masaa ya Afrika Mashariki. Ile notisi ya ‘we are coming soon’ bado ipo, ila ni kwa sababu tunafanya majaribio kem kem kuhakikisha kuwa kila kitu iko timaam, kabla ya kulaunch kwa mara nyingine tena.
Ili tusije tukapotezeana muda bure tafazarini watu wa kudeclare damu status mara kwa mara, tumewasikia - hakuna haja ya kurudia. Watu wa kusema nimehama/ninabaki, haina haja. Ongea kwa vitendo
Mwisho ni kwamba tunatafuta modareta. Preferred candidate ni yeyote ambaye ako na good communication skills, and social media presence. No Cv required. Kazi itakuwa ni kumoderate forum, handling our PR, na maintaining/updating our social media platforms. Wasiliana nasi kupitia barua pepe, [email protected] kwa walio interested
Ni hayo tu kwa sasa, shuqraniini, na muwe na jioni njema