4 ships with a carrying capacity of over 2,000 tons each begin operations from Tanzania - DRC Lake Tanganyika

PROFESA MBARAWA ASEMA BANDARI YA KAREMA KUWA CHACHU YA MABADILIKO MAKUBWA YA KIUCHUMI KATIKA MIKOA YA KATAVI NA KIGOMA.

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Novemba 21, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa meli nne za mizigo katika Bandari ya Karema, mkoani Katavi. Ujenzi huo unatekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ushirikiano na kampuni binafsi ya Nzenching International Company, ambapo kila meli itakuwa na uwezo wa kubeba tani 2,000.

Prof. Mbarawa amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika mikoa ya Katavi na Kigoma, huku ukiwa na uwezo wa kuzalisha ajira zaidi ya 6,000 hadi 7,000.

“Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ili kuongeza tija, ushindani na fursa za kiuchumi kwa wananchi,” amesema Prof. Mbarawa.

Amesema kuwa kukamilika kwa meli hizo kutawezesha usafirishwaji wa mizigo kutoka Bandari ya Karema kwenda DRC, pamoja na kuelekea Kigoma na Bandari ya Dar es Salaam, hatua itakayoongeza biashara na kuimarisha nafasi ya kiuchumi ya ukanda wa Ziwa Tanganyika, ikijumuisha pia nchi ya Zambia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, amesema kuwa ushirikiano kati ya TPA, TASAC, na taasisi nyingine za Serikali umewezesha kusukuma mbele utekelezaji wa mradi huo, ambao utaimarisha mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Karema hadi Kigoma na Dar es Salaam, pamoja na kuchochea kasi ya ujenzi wa reli na barabara kutoka Mpanda kwenda Karema.

Naye Mhandisi Said Kaheneko kutoka TASAC amesema kuwa michoro ya meli hizo ilikaguliwa na kuidhinishwa kabla ya kuanza kwa ujenzi, ambapo kila meli ina urefu wa mita 70 na upana wa mita 15, na itakuwa na alama maalum zitakazoonyesha ikiwa mzigo umezidi kiwango kilichowekwa.

hio ni kama boat ya fishing kidogo sana

Aisee, @255 mumezikana?

poo GIF