Tahadhari kwa Villagers Wanaotoka Jamii Forums.

Kaka mkuu

Senior Villager
#21
mnaopenda siasa ndio mpo mahala pabaya mno ila mie mpenda ngono natafutwa kisa nini sasa
Kuna kosa la cyber crime linakunyemelea, kosa sio kutukana wenye mamlaka hata kutukana yeyote au kutumia lugha yoyote isiyobalika na isiyo na maadili bado ni kosa LA jnai.


Kaka
 

chinga one

Senior Villager
#27
Hii ni kwa Villegers wote ambao hatuna uelewa wa it na wanahisi michango Yao na post Zao wenye mamlaka hawapendi kusikia au kuzisoma
Kama tunavyojua teknolojia kwa wenzetu imekuwa ushetani ndo maana wakaomba Maraika toka juu washuke kuja kufungia mitandao, ni hivi juzi tumeshuhudia Ombi likijibiwa kwa namna ya pekee mpka sasa tupo uhamishoni.
Mambo ya kujiuliza
1.
Usalama wetu upoje huku ugenini?
2. Je adui yetu ameridhika na hatua tulizo zichukua ili kujikomboa?
3. Adui zetkiteknolojiawamejipangaje 4. Nini cha kufanya ili uwe salama?
Hivyo basi lengo si kujibu maswali yaliopo hapo juu kama wengi mlivyotarajia ila ntajikita katika jambo moja tu, Kwani yapo mengi ya kufanya ili kujilinda ila tuanze na hili Leo.
Kwa kipindi chote ambacho tupo huku ugenini ni vyema tukachukua tahadhari popote pale uwapo. Kumbuka kuunitick pindi unapo sign in pia usisave password kwenye browser unayoitumia, hii itakusaidia pindi ukikutana na wasiojulikana na wakachukua simu yako na kuipigakuisearch.
Nibora ukatunza password na username yako kichwani kuliko kuiacha ikwa inainasign automatically.
Nawasilisha.
Tena kwa wale ambao wamehusika kusambaza link ya jamii forums kupitia KenyaTalk kwenye Wasap groups wachukue tahadhari hii....the fact is wanafatiliwa kimya kimya.
 

COARTEM

Senior Villager
#33
Tatizo kuna mavileja hawajatosheka na kufungwa kwa JF sasa wamegundua kwamba huku hawana ubavu wa kufungia huu mtandao ndiyo wamebakia kututisha!
Uoga wetu ndiyo umaskini wetu.
Humu hatumtukani mtu, ni just freedom of expression.
Unajuwa ni sawa na mwanamke ndani ya nyumba ukimzuia kuongea ipo siku atakuja fanya tukio usilolitarajia.
Mtu akiongea anatoa nyongo zake yanaisha.
 
#34
Suala la username na password hata ukitumia JF original App au browser lipo palepale (Hakuna tofauti na huku ugenini).

Labda tujadili vigezo na masharti ya KenyaTalk kuhusiana na usiri na usalama wa taarifa zetu.
 

Top