Nianze kwa kunukuu vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muunhano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005, ibara ya 3(1) ambayo inasema “Jamhuri ya Miungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi” mwisho wa kunukuu
Duniani kote kwenye nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi, tafsiri yake ni kuwa vyama vya upinzani, wajibu wake mkubwa ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani ili ijirekebishe na kuwatendea haki wananchi
wake
Hebu ninukuu Ibara ya 18(1) ya Katiba hiyo hiyo ambayo inasema " Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia Uhuru na mawasiliano hayo hayapaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote" mwisho wa kunukuu
Nimejaribu kuvinukuu vifungu hivyo viwili ili tuone huyu Rais wetu anavyoisigina waziwazi Katiba ya nchi ambayo kabla ya kuingia madarakani aliapa kuwa ataitii Katiba hiyo
Kuhusu mfumo wa vyama vingi ni wazi kuwa wanachofanya viongozi wa upinzani kwa kuikosoa serikali iliyoko madarakani, ndiyo wajibu wao namba moja kwa wapiga kura wao
Tujiulize inakuwaje kiongozi wa upinzani anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi, Jeshi la Polisi linamkamata kiongozi huyo na kumfungulia mashitaka ya uchochezi??
Tunajua kuwa Rais wetu Magufuli hataki kabisa kukosolewa, lakini Jeshi la Polisi linapaswa lifanye kazi yake kwa weledi wa kutojiegemeza na Chama chochote cha siasa na sivyo wanavyotekeleza wajibu wao kwa hivi sasa ambapo huwezi kuwatofautisha na UVCCM!
Tuje kwenye ile ibara ya 18(1) ya Katiba ambayo inatoa Uhuru kwa kila mwananchi kutoa maoni yake. Hivi tungeweza kweli sisi wananchi wa Tanzania kuwa wakimbizi nchini Kenya kwa ajili tu watawala wetu wameamua kuisigina Katiba ya nchi??
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi, hivi inakuwaje kwa Rais wa nchi kuamua kuisigina Katiba ya nchi waziwazi, ambayo kabla hatujamkabidhi madaraka hayo aliapa kuwa ataitii na kuilinda Katiba hiyo??
Nimekuwa pia nikijiuliza hivi huyu Rais Magufuli anapata wapi kiburi cha kuisigina Katiba ya nchi waziwazi??
Jibu ninalolipata ni kwa kujiona kwake kuwa ndiyo Commander in Chief wa majeshi yote nchini, kwa hiyo wapinzani hata mkiamua kuprotest kuhusu utawala wake, yeye ataviagiza vikosi vyake vya Polisi vije na magari ya washawasha ili viweze kuzima maandamano hayo!
Lakini kitu wanachosahau hayo majeshi ya Polisi ni kuwa hayo magari ya washawasha yananunuliwa na pesa za mlipa kodi wa nchi hii na mishahara ya hao Polisi inatokana na “kujisachi” mifukoni kwa tax payers
Kitu kimoja kilicho cha wazi ni kuwa kama kweli Bunge la nchi hii lingekuwa linafanya kazi yao wanayopaswa kuifanya ya kuisimamia serikali, basi lingekuwa limeshapiga kura ya kukosa imani kwa Rais wa nchi hii siku nyingi sana na Rais huyu angekuwa ameshatuachia huo Urais wetu
Ee Mwenyezi Mungu tujalie waja wako watanzania, na utuondolee huyu Magufuli ambaye ni dhahiri ame-abuse power yake