Comment mpya toka kwa Max Melo kuhusu kurejea kwa JF

Kupitia ukurasa wa JF kule insta max akijibu swali la mdau wa JF ametoa matumaini ya JF kurudi hewani. Comment ya melo hii hapa:

@macdemelo
1 day ago
@_tununu tunasikitika kuwa imechukua muda mrefu kurejea tofauti na matarajio yetu. Hata hivyo, tumefikia hatua nzuri inayoashirikia kuwa muda si mrefu tutarejea hewani tukiwa imara zaidi. Ombi lako la posts kuonekana hata kama mpya zisipoingia linafanyiwa kazi pia

kuna njitu humu zimeiba ID za watu jf halaf wanatusua nazo humu na kule BF lahaulaaa hawajui kama zinasakwa na tcra/lumumba, hapo ndo utashangaa mwiz anakiri kuiba na alieibiwa anakana kuibiwa hahaaaaa. M simo yan n sawa na kutoboa meli haraf umo ndani.

Kama watarejea kwa masharti hayo hayo(Kuendelea kuendesha shughuli zao hapa hapa nchini) basi watu wengi kwenye jukwaa la siasa watabakia kuwa wasomaji tu.
Ila kama wamehamisha Ofisi (kuweka nje ya nchi) basi itaendelea kuwa imara zaidi na watu wataendelea Kuchangia kwa Uhuru zaidi.

Wameshakandamizwa weee ndo
Wanarud

Haya mambo ya kutoa ahadi,kisha hazifiki,sio vizuri kabisa…

Warudi bana

Hata wakirudi sidhani kama watakuwa huru kama mwanzo…

Hata wakirudi na huku tutakuja kama kawa

dah hv karbni! lets wait

Tuna subilia kwa hamu na jamu

kama watarejea, wapunguze censorship. waache watu wafunguke.sio mtu umejipinda kuandika thread inayohusu jambo fulani linalohusu serikali, halafu baada ya dakika chache, moderator anafuta au anakupa ban.

[quote=“Usser, post:4, topic:164765”]

Wameshakandamizwa weee ndo
Wanarud
[/QUOTE

ndo Tz yetu bby[/QUOTE]

Yote kwa Yote ule uhuru wetu wa kutoa maoni kama inavyoainishwa Kwenye katiba ya JMT haupo tena

@innaa Bby Sasa kwa maisha haya
Tutapumua kweli

Me naona Bora tuhamie huku Kwa Kenyatta

Hilo ombi la kuachilia post za zamani bila kupost kitu mimi pia naliunga mkono.

Woga wenu tu, mbona jamiiforums michango yake ni ya kistaarabu kuliko mitandao mingine kama facebook na instagram?JF ukiitukana serikali au kiongozi moderator wanafuta au ku edit, mitandao mingine ya kijamii watu wana comment matusi na kejeli wala kukamatwa hawakamatwi

Itapendeza sana…

Cc: @Mahondaw

Mi hapa pananitosha

[FONT=courier new]Sema utakuja na usiseme tutakuja tafadhali. Lini tumekuteua kuwa ’ Spokesman / Spokeswoman ’ wetu?[/FONT]

kweli kabisa bby tuhamie huku haya manyanyaso ya Tz sio kabisa