Chapat za kusukuma ni janga au changamoto kwa wanawake/wasichana walio wengi
Chapat za kusukuma ni kuukanda unga vizuri had yale mabonge bonge yasiwepo yan unga uwe smooth pia usiubwabwarize maji yan usiuzidishe maji uwe mtepe wengine wamekremisha chapat had uzichemshie maji
Mimi hua nafanya had za maji baridi na zinakua laini
Hata hivo chapat usizinyime mafuta yasiwe mengi had yajifyonze kiasi tu yanatosha kwenye kukunjia chapat had kuzikaanga kwenye chuma chake[ATTACH=full]178031[/ATTACH]
Kuandaa mtura
Chukua utumbo ule mkubwa wa mbuzi au ng’ombe usafishe vizuri.
Katakata nyama vipande vidogo vidogo sana, katakata vitunguu carrots na hoho (shape ya square).
Changanya vipande vya nyama na hivo viungo (Carrot hoho na vitunguu) na chumvi kisha weka katika ule utumbo mkubwa, funga utumbo ili visimwagike choma na moto kiasi, vitadondosha maji hadi vikauke.
ni mtamu kwakweli kwa Arusha pale Kenny garden ukifika mlangoni utasalivate.
Dar nishapata mara moja pale kumekucha kwenye mbuzi mtura pia unapatikana.
home made mara moja moja
Kanda unga kwa muda mrefu hadi uwe laini, uchanganyikane vizuri. Uunga uliokandwa vizuri muda wa kusukuma huwa unatokea vi bubbles (unajaa kama vile unavopuliza big G ) hapo ujue unga upo vizuri.
Wakati wa kukanda usiweke maji mengi hadi unga uwe mtepe kisha uanze kuongeza ongeza unga kuufanya uwe mgumu, chapati zitakua ngumu.
Weka maji au kimiminika kidogo kidogo hadi kitoshee
Wakati wa kukaanga chapati, usikaange na moto mdogo sana.