ZANZIBAR VIJANA WAHAMASISHWA KUOA WAJANE

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Asha Suleiman Iddi amesema wajane wengi wanaweza kuondokana na changamoto zinazowakabili iwapo vijana wataamua kuwaoa.
Iddi alisema hayo katika utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano ya kaswida yaliyoshirikisha madrasa 13 za Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema wakati umefika kwa wanaume kuona umuhimu wa kuoa kutokana na kuongezeka matukio ya ubakaji ambayo yanaitia aibu nchi.
Iddi alisema jambo baya zaidi ni kuwa vitendo hivyo sasa vimehamia katika maeneo ya kusimamia masuala ya dini yakiwamo madrasa na misikitini, jambo ambalo linaifanya jamii kukosa amani katika maeneo yao.
Alisema inasikitisha kuona hali hiyo ya ubakaji ikitokea kwa watoto wenye umri mdogo, wakati kukiwa na kundi kubwa la watu wenye kuhitaji waume wakiwamo wajane.

Watu tunataka dogo dogo (vitu fresh).

Hao “wabibi” nani anawataka?

Watoto waliowazaa nani atawalea??..muoaji au??

Hahahha hiyo n applicable huko zenji sio huku bara

Tena unakuta mtu anasema kabisa siwezi date na single mother huku yeye analelewa na baba wa kambo

wazenji wanawataka

jibu ilo

Hili nalo neno mmmhhh :skull_and_crossbones::skull_and_crossbones::skull_and_crossbones:

Umeona eh

Duuuu hiyo nayo ni nzuri huko kwao ila kwetu ni hatari

Kwani mabinti chipukizi wameisha au wamebaki wachache? Labda awe anakuja unasuza rungu anaondoka ila kuoa :rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:

Tatizo ni baba wa huyo mtoto kama yupo alive, wanaanzaga kujifanya wazazi baadae migegedo inaendelea afu kidume ndio unalea. SHUBAMIT!!

Inaonekana hali ni mbaya sana kuliko tunavyofikiria,idadi ya wanawake wasio na wanaume na wanahitaji kuwa nao imekuwa ikiongezeka kwa kasi ya ajabu,serikali ifanye jitihada za makusudi ili kurekebisha haya mambo…

Sio mbaya

Uache kula nyama fresh ule kongoro?

Siku hizi ndoa kwa Dada zangu ni Bahati ukiipata shukuru maana wanaohitaji ni wengi sana.Hata matangazo ya kutafuta wachumba mengi ni ya kwao.Kinachosikitisha umri wengi ni miaka27-40.Na hii inafuatia kwa wengi wao kuchagua na kuwadharau wanaume wengi waliowafata kwa ajili ya kuwaoa mwanzo na hatmaye kutumiwa vbaya usichana wao na kuachwa kwenye mataa.Ushaur Dada zangu,majigambo dharau vina mwisho wake.NDOA NI SHERIA LAKINI MNAKUJA KWA WENGINE BAADA YA KUCHEZEWA SANAAA

Serikali imeisha sema watu waache kubaka na kuoa wanawake wasio na wanaume au wajane,hakuna cha ziada ambacho serikali inaweza kufanya

Asilimia kubwa ya wajane ni watu wazima, sasa vijana tena wakiwaoa si itakua kama wanaoa mama zao…

Cc: @Mahondaw

Waje na huku bara