Waziri Mpango hufai kuwa waziri wa fedha jiuzulu

[ATTACH=full]178647[/ATTACH]

Sasa hivi kiongozi yoyote hata asiwe na uwezo nafasi yake ni salama ili mradi anamnyenyekea mkuu na kumsifia, basi nafasi yake ni salama.

Mkuu huyo ndio anaekwenda kuumalizia kabisa Uchumi kidogo wa Tanzania uliokuwa umebaki…
Dr Mpango ni zaidi ya Bomu.

ukisoma hotuba ya bajeti ya 2018/2019 kurasa kibao za kwanza zimejaa sifa na utukufu kwa jiwe, sijui ndio protocal au ni uoga au ni njaa?

Yaani mtu umeishakuwa Profesa, yaani bado una njaa kiasi hiki kweli?

Wasomi wana historia mbaya sana na siasa za nchi hii. Na hii serikali imesheheni wasomi, but unfortunately mambo yanaonekana kuwaendea kombo kila siku.

Labda tuwape bado muda wa kutosha kuwapima kabla hawajarudishwa kunakowafaa kwenye tafiti na maandiko yaliyojaa nadharia nzuri nzuri.

@FILIPO MPANGO.

Nadharia yote aliyoiweka akiwa Tume ya Mipango ameipiga teke na sasa anataka kuivunja kabisa Tume hiyo! Sasa tumueleweje?!

Huyu ni mchumia tumbo tu anafuata akili ya bosi wake!!

Kama jiwe tayari linajua ni nini kifanyike sasa tume ya nini? Wafute tu wakajipangie wanachotaka kufanya ikulu basi.

FIKAJAPO MPANGO!

Mi naona mnamuonea tu Mpango, yeye anaandika anachoambiwa na boss wake. sasa mnataka aandike tofauti atumbuliwe! kwani yeye mjinga

Mkuu hakuna watu wanaogopa maisha kama wasomi. Ukitaka kuamini nenda mahali tajiri hajasoma kisha akaajiri msomi ili amshauri kutokana na elimu yake. Dakika ya mwisho utakuta msomi ndio amegeuka kushauriwa na boss wake na msomi hugeuka mtu wa ndio mzee.

Hebu jaribu kuangalia mambo wanayoyafanya akina Prof. Kabudi ni aibu. Unakumbuka Prof. Kitila alivyopewa ukatibu mkuu wa wizara ya maji? Alikuwa anapandishwa majukwaani kama kiongozi wa siasa na kuanza kumwaga ahadi hewa, akafikia mahali eti anasema atamtafutia Magufuli kura!! Sasa katika maziingira haya mtu anaweza kutoka akasema wasomi wanajitambua au wanapigania matumbo yao?

Hii picha inanipa maono ya hali halisi ya viongozi wa awamu hii baada ya kumalizika kwa awamu na kuja awamu nyingine.
Nawaona wengi sana katika hali hiyo. Wakikabiliwa na kesi za uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka, huku katiba ikiwa imelitenga Jiwe na kuliegesha pembeni likifurahia kinga.
[ATTACH=full]178718[/ATTACH]

Pengine ni maagizo kutoka juu.

Jamaa anafanya mipango kabambe kugombea ubunge uko kigoma uchaguzi ujao

hi

hivi hawa jamaa waliingia BOT wakachukua fedha kwa mikono yao,siwalipewa na wenye madaraka asa iweje wateswe wao,hawa ni kama vibaka waliotumwa na tapeli kuu ambalo linakula maraha mpaka sasa

Aisee safari hii tutashuhudia mengi

Yajayo yanasikitisha sana
Nalog off

Kweli kabisa hill jiwe linakwenda kujitwalia madaraka yote

Hii picha inasikitisha sana,ndio hawa watu ni wahujumu uchumui,lakini sifikirii wanatafauti na akina Chenge,Rostam Aziz,na wengine,kwanini hawa watu hawatendewi haki,kwanini mahakama inawatesa kiasi hichi