Wakuu, najua tuko katika wakati mgumu sana kutokana na uongozi wa jf kuamua kuifunnga jf kutokana na sababu ambazo zimetolewa na mamlaka. Lakini kutokana na uraibu tuliokuwa nao tumeamua kuja ugenini ili angalau tupunguze misongo ya kutoweka kwa jf. Lakini tangu tuje huku kuna jambo moja ambalo kwa namna moja au nyingine linakuwa ni changamoto japo kwa nyakati nyingine linaweza kukuacha na tabasamu, ni aina ya kiswahili wanachozungumza wakenya…ni tofauti sana na inakuwa ni ngumu kuelewa ni nini hasa kinamaanishwa. Sasa ili tuweze kuendana na wenyeji wetu tusaidiane jinsi ya kuifahamu lugha yao kidogokidogo.
Mod naomba urekebishe heading…siyo tunifunze bali ni tujifunze
Sawa tutajifunzanga
ugali kukuja pande hii,
Akimaanisha nini haahaa
Hahahaha
Nao chakwetu hawakielewi wanasema mpaka watumie physic nyingi.
Hahahaha yan nacheka wanavyoandika mfano gusa eti ni gusa wanatukana hao ingekua jf saa hizi ban zimetembea kama karanga
Mi napenda kiswahili chao…ila kinachekesha
Swafi msupa
Hii yetu ni sheng, sio kiswahili
Hiyo sheng Tanzania inaitwa swanglish naona mnachanganya tu English swahili na lugha zenu za mashinani hahaha lugha za kigatuzi
Tunatakiwa tuhamie nacho Kule ili hata tukiandika chochote kile wasiojulikana washindwe kutuchukulia hatua.
Ukweli wa yote kiswahili fasaha kinatokana na lahaja ya kiunguja ambayo ndiyo imesanifiwa na TUKI ambayo siku hizi inatambulika kama TATAKI. Ni kabla ya uhuru wa Tanzania
Kiunguja ndiyo hiki kinachozungumzwa Tanzania, sasa tutaachaje lahana fasaha na kujifunza isiyo fasaha. Wao ndiyo wanapaswa wajifunze lahaja yetu.
Sahihi kabisa
yaani mamae, hata ile avatar yangu ya JF nimeshindwa kuipata
Waaaiii
Jamiiforum tunayo hebu hatuna?
Tujifunze kiswahili mbofmbof ya nini wakae ni kiswahili chao kwenye majukwaa yao n
#mgenianagubu
Kenya hakuna kiswahili… wao ndiyo wajifunze chetu…
Ni sawa na useme tujifunze kiswahili cha Congo…
Cc: @Mahondaw