Natembelea sana Nairobi mara kwa mara.
Ilikuwa mwaka jana ndio kwa mara ya kwanza nafika Nairobi. Nilikuja kwa Bus ya Dar Lux.
Kwa bahati nzuri nilikaa siti moja na Dada wa kikenya ambae alikuwa amekuja Dar kwa mchizi wake ambae ni Mtanzania.
Uzuri nilicho wapendea Watoto wakikenya ni kwamba, wako shapu na hufunguka kwa swali lolote unalo mwuliza, tofauti na dada zetu wa kibongo.
Ilibidi nimwulize ilikuaje akajenga mahusiano na mtanzania? , Ni mazingira gani yaliwafanya mpaka mkawa pamoja.
Aliniambia walikuja Tz ktk program ya kijamii, ambao ilikuwa inahusisha wanafunzi wa kule na huku. Sasa wakawa wapo field hapa Dar, na walipangishiwa hostel ambao walikuwa wanaishi wanafunzi wa Kikenya na Tz.
Ndipo alippkutana na huyu Mtz. Anasema alichompendea huyo jamaa ni kwamba, alijuwa romantic, anajali, na anaupendo wa kweli. Alienda mbali na kusema kuwa huyu jamaa ndio alokuwa mwanaume wa kwanza kumtunuku bikira yake. Dahh!
Dada akafunguka zaidi akasema kila baada ya miezi miwili lazima aje bongo kukutana na mchizi, na hata siku ile alikuwa kaja bongo kwa wiki nzima na ndo alolikuwa anarudi.
Tuliongea mengi sana, mpaka tukafika Nairobi na kuagana. Nilifikia hotelini.
Nikiwa na mishemishe zangu Ndani ya jiji, niliingia duka moja la nguo niweze nunua sweta. Nilikutana na mdada wa kikenya ambae ndie alikuwa anauza. Kama kawaida nilinunua sweta kwa Ksh 1500.
Niliona haita kuwa haki hata mbele za Mungu kumuacha mtoto mzuri kama huyu bila kuchukua namba yake. Bila ajizi wala usumbufu, nilipomwomba yule dada namba yake alinipa kwa unyenyekevu kabisa.
Kufupisha stori, haikupita wiki yupe dada nilidate nae na kujenga mahusiano. Yeye ndie alikuwa kipenzi changu kila nikija Nairobi.
Kwasasa tumeachana kutokana na dada kupenda sana ela. Yani wakenya sijui mkoje, yani mnapenda ela si kitoto, alafu ela zenyewe si zakawaida. Just imagine mtu anakuomba Ksh 5000 kama anaomba pipi, alafu simple tu.
Hiyo Ksh 5000 ni zaidi ya Laki moja. Huku Tz Ksh 500 demu inabidi ajibebishe sana, na tena aimbe kwelikweli.
Ila nilichokipenda kwa madem wa huko, akisikia wewe ni Mtanzania achomoii.
Nawasalim