UMUHIMU WA MSHAIRI KUSAJILI KAZI YAKE.
Julio cha wizi wa kazi za sanaa kimekua kikubwa sana nchini Tanzania na hasa kwa wakati huu ambao nao wasanii wa fani ya ushairi wanazidi kukua katika jamii ya watanzania.
Kwa muda mrefu,sanaa ya ushairi ilikuwa imepoa sana hasa baada ya kuingia kwa sanaa ya muziki wa kuzazi kipya ambao kiujumla nao umeleta madhara Fulani kwa sanaa halisi ya mashairi hususani haya ya kimapokeo.
Kwa Mara kadhaa kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya washairi kuibiwa kazi zao na kilio cha wizi wa kazi zao kimekua kama kilio cha samaki ambacho siku zote hupotelea majini.
Kwa Mara ya kwanza kiasi cha wiki kadhaa zilopita niliahidi kuandika katika blog yangu kuhusu “Umuhimu wa mashairi kusajili kazi yake” lakini kutokana na muda kuwa mdogo wakati mwingine nilishindwa kufanya hivyo.
Ila kwa Leo nachukua nafasi hii kuandika makala hii fupi ambayo pia nitaelezea ni jinsi gani washairi wataweza kusajili kazi zao.
Kwanza nianze kwa kusema haya,japokuwa yataweza kuonekana kuwa ni maneno mabaya kwa baadhi ya washairi.
Kwanza,washairi tumekua ni watu wazembe katika kufuatilia kazi zetu na sanaa yetu.
Washairi wengi hasa wa Tanzania tumeridhika na kuishia kutunga katika magazeti,mitandao ya kijamii na MTU kama akiandika kitabu anaona ndio basi Keisha kamilisha kazi kubwa ya ugwiji wa ushairi.
Ila niseme hivi,sasa hivi dunia imebadilika kwa kiasi kikubwa,mteja ama mdau au mwanajamii haifuati sanaa yako wala tungo yako balibwewe msanii na mwanataaluma wa sanaa Fulani ndie unaetakiwa kumfuata mdau wa sanaa yako.
Ukikaa nyumbani na kuishia kutunga katika mitandao ya kijamii hakuna kitakachopatika Bali wanajamii wataendelea kuamini kuwa Ushairi ni sanaa ya wazee kwa kuwa wengi wengi walisoma mashairi yaloandikwa na watu wa zamani na siyo wa sasa.
Hiyo siyo mada yangu sana ila nilikuwa nataka tuzinduane hapo.
Mada yangu ya Leo umuhimyvwa sasa kama washairi kusajili kazi zetu.
Kazi yeyote ile ambayo ili iwe na hati miliki ya kwako ambayo itakulinda na kukuza hali kama mashairi,ni kazi ambayo nitakuwa tayari imesajiliwa katika chama cha “cha hakimiliki Tanzanian” ambacho kinajulikana kama “COPYRIGHT SOCIETY OF TANZANIA” ama “COSOTA” ambacho Lengo la kuanzushwa kwake ni kusimamia hali miliki na kumlinda mwanachama dhidi ya wizi wa kazi hasa za sanaa.
Kwa Tanzania,ofisi za chama hiki zipo mkoani Dar es salaam katika BARABARA ya Chato plot namba 271.
Ni halali kwa mshairi wa Tanzania na nje ya Tanzania,kuwa mwanachama wa Cosota,ambae ataweza kujiunga na KUWA mwanachama na kusajili kazi kazi zake hapo ambazo mwisho wa siku zitakuwa katika ulinzi madhubuti wa mwezi wa sanaa,ambao wakithibitika kuwa ni wezi wa kazi za sanaa basi sheria itachukua mkondo wake,ila kama hujasajili na kazi yako ikaibiwa,itakua imeangukia pabaya kwako maana hakuna wakukutetea kwa hilo kwa sababu moja,hukuhifadhi kazi yako sehemu salama.
Mbali na usajili wa MTU mmoja moja,pia kikundi cha washairi Wanaweza kujisajili kuwa wanachama wa Cosota na kupata haki miliki zao.
Mfano kwa hapa Tanzania vikundi kama “Arusha poetry club” na “Majagina wa ushairi” wana nafasi kubwa ya kujisajili na KUWA wanachama wa Cosota na SIYO Cosota tu,hata Basata pia.
Ila kama nilivyosema mwanzo,washairi hasa wa Tanzania tumeridhia sana kuishia mitandao ni.
Kwanza,kazi kama kazi ya msanii ili aweze kusajili wa kazi yake,ni lazima awe mwanachama wa Cosota na kusajili kazi moja ni shilingi elfu moja tu,je ni Nani atashindwa hapo na je ni Nani atakae lalamika kuwa ameibiwa kazi yake.
Tutaona mbele hiyo elfu moja inakuwa vipi na hali kutakuwa kuna umuhimu wa Yale nilisema mwanzo kuwa tumeridhika kuishia mitandao ni.
Ili sasa KUWA mwanachama wa Cosota kuna mambo yafuatayo ya kufanya.
KWA MTU BINAFSI.
Kwa shairi binafsi,utahitajika kulipia gharama kidogo ili kuwa mwanachama (hii inamuhusu mtanzania).
Ada ya fomu ambayo ni shilingi elfu kumi pamoja na ada ya mwaka ambayo nayo ni shilingi elfu ishirini ambazo kiujumla ni shilingi elfu thelathini na uanachama wako unakua umekamilika.
Kama mnasajili kikundi cha washairi,mtafanya yafuatayo
Mtalipa ada ya fomu ambayo ni shilingi elfu ishirini na ada ya mwaka ambayo ni shilingi elfu themanini,je kuna kundi la washairi hadi hapo litashindwa kuwa mwanachama wa Cosota.
Vile vile kama nilivyosema mwanzo,mbali na mtanzania hata asie mtanzania anaweza kujisajili kuwa mwanachama wa chama cha haki miliki Tanzania.
Nao pia kuna gharama zao kidogo.
Ada ya fomu ni shilingi elfu ishirini na ada ya mwaka ni shilingi elfu ishirini,jumla ni shilingi elfu harobaini ambazo kwa mshairi wa Kenya atalipia kiasi cha shilingi elfu mbili za Kenya kwa kupata usajili wake na kama ni kazi atalipa shilingi shilingi mia moja ili kusajili kazi yake ya ushairi.
Kama kikundi cha ushairi nchini Kenya kinataka kuwa mwanachama wa Cosota kitafanya yafuatayo.
Kitalipa ada ya fomu ambayo ni shilingi elfu harobaini na data mwaka ambayo ni shilingi elfu themanini na ujumla wake ni shilingi laki moja na elfu ishirini.
Wakati wa kuomba usajili wa mwanachama,muombaji anatakiwa kufanya yafuatayo.
Juan nation sha picha yake mdogo,yani paspoti saizi mbili.
Cheti cha kuzaliwa ama kitambulisho
Majina ya warithi wake wa badae,pamoja na picha yake,kitambulisho ama paspoti.
Taarifa zako za bank ,pamoja na mawasiliano yako,namba zako za simu,barua pepe na kadhalika.
Kama washairi mnataka kusajili kikundi,mtaambatanisha mambo yafuatayo.
Majina ya wanachama wenu na wawakikishi wao.
Picha wanachama wenu.
Nyaraka za kikundi chenu kama leseni ya biashara,cheti cha Baraza la sanaa Tanzania (Basata).
Katiba ya kikundi chenu.
Iwapo mshairi ama washairi watafanikiwa kujisajili hivi,basi mshairi utaruhusiwa kumpeleka mwizi wako Cosota na sheria nyingine zitafuata hapo.
USHAURI WANGU KWA WASHAIRI HASA “UWASHATA”
Kama chama cha washairi Tanzania ni wajibu wenu kupeleka kilio hiki kwa serikali.
Waambieni washairi wa Tanzania wanahitaji kusajili kazi kwa mfumo mrahisi.
Mfano,kama mshairi hajaandika kitabu,basi aweze kuruhusiwa kuyakusanya mashairi yake katika chapisho la kawaida na asajiliwe kwa bei ndogo kwa kuwa wengi wa mashairi wa Tanzania hawajaanda kufanya ushairi kama biashara.
Leo hii msanii wa muziki hata akiwa na nyimbo moja anaweza kuimba jukwaani na akalipwa na akasikia kata dunia nzima lakini mshairi hawezi andika shairi mtandaoni na likasikija duniani mzima kwa sababu washairi bado hawajapata wadau wa kubwa wa kuwasukuma mbele.
Cha cha washairi Tanzania ni wajibu wenu sasa kuwakutanusha kwa wingi washairi wenu na kuzikabili changamoto zao na kutatua matatizo yao.
Kuwapa elimu juu ya Kazi zao na umuhinu wa wao kujisajili baraza ka sanaa Tanzania na SIYO kubaki kila siku kukosoana katika makundi ya WhatsApp na mitandao mingingine ya kijamii.
Ni wajibu wenu kuwafanya washairi wajisikie ni watu wenye thamani katika jamii kwa kazi zao kuonekana katika jamii ya wa Tanzania,na SIYO kupokea changamoto za ndani ya makundi ya WhatsApp pekee ambayo bado hayana matokea makubwa ya moja kwa MOJA kwa mshairi.
Leo ni aibu kubwa sana tena kubwa isiyo na kifani kwa mshairi kulalamika Mara zaidi ya tatu kuwa anaibiwa kazi zake na nyie kama chama cha washairi mkawa mpo kimya bila kusema chochote.
Jukumu la kuwasimamia washairi katika masilahi yao ya moja kwa MOJA ndio jukumu lenu kubwa mlopewa kwa ajili ya washairi wenu na kizazi cha ushairi cha baadae.
Hamtoweza kulinda ushairi wala lugha ya kiswahili kama hamtoweza kusimamia haki za washairi wenu.
Hamtoweza kulinda ushairi,washairi na kiswahili kama hamtjitolea kujulikana na jamii.
Moja ya jukumu lenu la sasa SIYO kuwafata washairi sana Bali ni kuwafanya washairi wenu waifuate jamii ili jamii iheshimu,ithamini ushairi na KISWAHILI.
Namalizia kwa kusema tena,“NI AIBU KUBWA KWA MSHAIRI KULALAMIKA KUIBIWA KAZI ZAKE HALI KUWA UWASHATA MPO NA MLISTAHILI KUWAELEKEZA WASHAIRI WENU NINI CHA KUFANYA”
Imeandikwa nami Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160