[FONT=courier new]Kwanza nianze tu kutoa pole kwa wale ambao mmepatwa na usumbufu juu ya hizi ID’s mbili. Kwa wale wana JamiiForums wenzangu ’ Brand ID ’ yangu ni GENTAMYCINE na siyo hii ya huyu ’ Popoma ’ iitwayo GENTAMYCIN. Labda niwataarifuni tu ya kwamba ni mapema sana leo ’ nilitonywa ’ na Mtu wangu muhimu kabisa kwamba kwakuwa JamiiForums imehamia huku Kenya na kwakuwa ’ michango ’ yangu kule JamiiForums ilionekana kuwa na mashiko, tishio na kukubalika sana kiasi kwamba najulikana na kufuatiliwa ’ Kimaudhui ’ na Watu wengi kuna Mtu mmoja ataharakisha upesi sana kuja na ID hii na ataweka hadi picha ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ( ambayo hupenda kuitumia ) ili aweze kuwachoteni akili zenu.[/FONT]
[FONT=courier new]Kuna wale Watu ambao mlikuwa mkiwaulizia Watu ’ wasiojulikana ’ ni akina nani basi leo naanza kumtaja mmoja wao kuwa ni huyu Member aliyeigiza ID yangu na kujiita @GENTAMYCIN na nilipomshindia na kumuweza ni pale ambapo ID yangu mwishoni inaishia na herufu ’ E ’ nikimaanisha ni GENTAMYCINE na hata katika Social Platforms zingine najiita Gentamycine Antibioutique.[/FONT]
[FONT=courier new][COLOR=rgb(235, 107, 86)]TAHADHARI.[/FONT]
[FONT=courier new]Huyu Member @GENTAMYCIN ni ’ asiyejulikana ’ kwa 100% na amekuja humu ’ Kuwahadaeni ’ hasa Members wale tuliokuwa kule JamiiForums ili mjue kuwa ni Mimi GENTAMYCINE ’ Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer ’ ili mjitusu / mkosee muwe mnachangia masuala ’ Nyeti ’ ya Tanzania kisha aweze kuwaombeni Urafiki halafu ’ awategeni ’ nanyi mkaokotwe Baharini mkiwa hampumui tena ( nadhani hapa mmeelewa namaanisha nini )[/FONT]
[FONT=courier new]Mwisho nikuambie tu Wewe ’ hopeless ’ @GENTAMYCIN kwamba hata ’ uigize ’ kila kitu kutoka Kwangu Mimi GENTAMYCINE bado hutoweza kuwa na uwezo wangu mkubwa wa mambo mbalimbali niliyobarikiwa nayo na Mwenyezi Mungu. Najua huko ’ Makao ’ ninawateseni mno ndiyo maana mnahangaika kupambana na hii ’ Brand ID ’ yangu kwakuwa mnaijua inavyokubalika, inavyoaminika na inavyopendwa na wengi.[/FONT]
[FONT=courier new]Kitendo chako tu cha ’ Kuniiga ’ ID yangu kuanzia Jina hadi Picha kumenisaidia leo kujua kuwa ama kweli GENTAMYCINE wa JamiiForums ni ’ Kiboko ya Jiji ’ na ni ’ habari ya Mjini ’ kwelikweli. Nakutuma unifikishie huu ujumbe kwa waliokuagiza kuwa mlipoamkia nyie leo Mimi nililala huko juzi halafu siku zote Nyoka huwa hazai Panzi bali Nyoka huzaa Nyoka na Nyoka anayezaliwa huwa ni ’ hatari ’ kuliko.[/FONT]
[FONT=courier new]Kwa wale wana JamiiForums nimeshatoa tahadhari Kwenu kwa huyu Mtu hatari ’ asiyejulikana ’ aitwae @GENTAMYCIN hivyo kuweni nae makini na Mimi GENTAMYCINE sihusiki nae kwa lolote na chochote na katika ’ Kuwazugeni ’ atakuwa anajifanya anaandika Kiswahili cha ’ Kikenya ’ ili muingie ’ mkenge ’ Kwake ila ni Mtanzania mwenzetu na yupo ’ Makao ’ na ameianzisha hii ID kwa ’ Kazi Maalum '.[/FONT]
[FONT=courier new]Nimemaliza.[/FONT]
[FONT=courier new]Nawasilisha.[/FONT]