Watu wa Dar JPM aliwapa bahati sana ya kuwapa Makonda kama RC kiasi ambacho sisi wa mikoani tunatamani huyu Makonda ambaye ninyi mnamuona ni wa kawaida ahamie huku kwetu. Japo RC Makonda ni kijana na bado hajawa na uzoefu mkubwa sana kiuongozi ila ameonyesha uwezo mkubwa sana tofauti na wale tunaowaona kama ni wakongwe kwenye uongozi. Nimesikia wengi wanaponda juhudi zake wakisema kila anachoanzisha hakifiki mbali, kama hili lina ukweli basi tatizo sio Makonda bali ni wale watendaji wa chini wamekosa uzalendo wa kusimamia kile ambacho RC amekianzisha.
Mfano; Suala la watoto wa nje, hapa RC alifanya alipoweza kufika, hii ilipaswa kuwa kengele ya kuwaamsha wafanyakazi wa ustawi wa jamii kuendelea pale RC alipoishia maana wao hasa ndio wameajiriwa kwa kazi hizo. Kama ni usafi wa jiji vivyo hivyo viongozi husika wa chini yake walipaswa kupokea kijiti hali kadharika ktk mambo mengine.
Binafsi natamani viongozi na watendaji wengine waige kutoka kwake.
Katika kampeni zake zote mfano za Shisha,Ombaomba,Usafi jumamosi,Kupiga muziki usiku,machangudoa,kuwasingizia madawa ya kulevya Manji na Mbowe nk ni ipi aliyofanikiwa?