Waigizaji wa kupima samaki migahawani waumbuka

Baada ya sakata la Maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuingia katika mgahawa wa Bunge na kukagua samaki kwa madai ya kupewa maagizo na Waziri wa wizara hiyo Luhaga Mpina. -
Spika wa Bunge Job Ndugai leo amesema >>>“Kwa akili ya kawaida watu wananunua samaki kwa kilo na sio kwa futi, sasa hii sheria ya kupima vitoweo hii…! Inabidi hizi sheria tuzisome vizuri, Watanzania wawe wanafunga milango ndio wale samaki”.
[ATTACH=full]178001[/ATTACH]

Hii ni aibu mkuu

Nipo ughaibuni yaani tunachekwa

Aiseee

Inasikitisha sana…

Wameonekana hawana akili…

Cc: @Mahondaw

Wanakataa kusomwa kwa bajeti ya kambi rasmii ya upinzani, wanajadili upimwaji wa samaki. Shenzi zao.

Hahah!! Samaki wafupi nikama madawa ya kulevya kwa sasa

Wana divert attention tu hawa.

hapa kazi tu

mbona movie ishaenda vizuri mkuu!

Mkuu tulio nje ya nchi yaani tunachekwa hatari hadi aibu

Taifa la majuha

Kutaka masifa na kujionesha wanafanya kazi … WATU WANAVYOONA KUNA KUPANDISHWA VYEO HADHARANI WANATUMIA FURSA…

Hiyo style waliyotumia hao maofisa ni copy & paste ya mkulu, jambo lisilo hata na tija linafanyika hadharani bila sababu ya msingi. Kama mkuu wao alipokea madiwani waliohama upinzani kwenye hafla ya kijeshi, itakuwa kwenda kupima samaki hapo kwenye bunge mateka wa serekali? Sioni bunge linalalamika nini wakati lenyewe limejipendekeza kwa serekali mpaka linashika maeneo ya siri hadharani. Hao maofisa wa serekali ndio huwa wanatunga sheria, kisha zinapelekwa bungeni na kupita kama zilivyo, sasa nani atawatisha wakiamua kuwashika makalio hapo bungeni? Tena inatakiwa na polisi waende wakatembeze mkong’oto hapo bungeni kwani hilo bunge ni kijiwe cha wahauni wasiojua nini wajibu wao.

Nabado tutaona mengi mwaka huu, laana ya ubadhirifu wao imeanza kuwapanda vichwani.

Kama wameanza kutumia futi basi watatumia hadi Pima maji

Ingewahusu wengine hata wasingesema, ubinafsi wa watunga sheria wetu wakiongozwa na spika, mara ngapi watu wanatozwa faini kwenye mabasi eti kakutwa na samaki wawili wa kitoweo, wanaotoka mwanza kuja dar kwa basi wanaelewa kadhia hii na haijaanza leo ila hawajawahi kuongea vile

HII NCHI HII VIONGOZI WANAAMKIA BAR NDIO WANAENDA OFISINI HIVI HATA UKIMUULIZA MKEO JAMBO UNALOKWENDA KUFANYA OFISI ATAKUSHAURI VIZURI TU MSILALE BAR

Leo nimeshindwa kununua samaki kwa kuwa mchuuzi wa samaki hakuwa na RULA sasa itabibi nikienda kununua samaki niwe na rula yangu maana yajayo yanatisha

Hiyo kitu ilipangwa na wahusika kutoka juu. Na wamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 70