Mimi nilikuepo huku kitambo sema sikujisajiri. Huku kulikua na Jukwaa la Tanzania News and Politics, ghafla likabadirishwa kuwa Jamii Forums huku ndani likibeba baadhi majukwaa yake.
Vinginevyo maisha bila ya jamii forums hayakunisumbua kabisa, nilisikitishwa na hatua lakini haikunipunguzia kitu
Siku ilikuwa kama mwaka vile
Mie kwangu yalikuwa magumu jamaani. Nakosa hata pakuanzia. Hahahaaaaa.
Na yote hayo ni mazowea ambapo kwangu jf kulikuwa ni zaidi ya nyumbani yaani mbali na fake id ila tulikuwa kama ndugu moja ambao tumekua na kusoma pamoja. Hahahaaa.
Hahaaa. Sema ukweli bana Mkuu.
Nilikuwa kama mgonjwa kwakweli siku ya kwanza,siku ya pili nikaanza kurukia tweeter,facebook na instagram ila haikuniondolea unyonge wangu.JF raha bana asikwambie mtu,umefika ofisi ya mtu unasubiria atoke unaingia JF,unapiga mzigo ofisi kazi zimepungua unaingia JF,umeingia hotel unasubiria order yako unaingia JF,umeshtuka usingizini JF…
Nilishaacha kununua Bando za Data. Nilishaanza kuchoka akili…
Nilishaanza kujiona blacked out!
Nilidata nafikiri maana nikaanza kuji register kwenye mitandao hata ambayo sikuwahi kuifikiria… Alosto mbaya sana
Maisha magumu bila JF
Ha ha haa…mbaya zaidi huduma zilikatishwa ghafla bila ya taarifa.
Tumepewa taarifa baada ya huduma kusitishwa
Mwanakijiji mwenzangu inabidi tukupeleke sober house maana hiyo addiction ni kiboko
Hahahaa. Umeonaee.
Yaan yanakuwa magumu mno rafiki.
Sasa wewe ume join jana tu na leo umeupata u-senior.
Ama kweli huku ni nchi ya kitu kidogo
Hahahaaa. Hiyo imetokana na Post zangu Mkuu. Hata weye ukifikisha ka hizo utakuwa Senior Villager.
Poleni sana…
Cc: @Mahondaw
Sana yaan JF raha sana
Nikisema yangu mtaniona mchawi ngoja nipige kimya
@Evelyn Salt tiririka tu mama…kuna wanao onekana mateja, mashankupe, washambenga n.k, so usiogope
nilikondaaaa mnoo yaani mpk nilitaka kujiunga na Facebook ila nimeghairi baada ya kujua huku
nimepanda citizen news pepa, nkakuta njia ya kufika huku…
ila melo bado nampa heshima hata kama nimekimbilia nchi ya watu
- Ghafla niliiona simu haina thamani tena.
- Bia nikinywa sii tamu tena na nalewa mapema
- Nawagombeza wafanyakazi bila sababu.