UTEUZI MWINGINE

Rais Magufuli ateua msajili wa vyama vya siasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Bw. Mohammed Ali Ahmed kuwa msajili wa vyama vya siasa badala ya Jaji Mutungi.

Shiiiiiiiiit

Mtungi kawaje.?

wakati mwingine wakigundua mnamchukia mtu na siyo sheria anayotumia mtu, hubadilisha mtu na kuacha sheria iko kama ilivyokuwa! Tatizo siyo mtu bali sheria ya kujinga ya kuwa na msajili wa vyama vya siasa. Hivi kusajili vyama vya siasa inakuwaje ni kazi ya muda wote!?

Kazi ipo

Nguruvi3 kule jamiiforums aliwahi sema hiki cheo ni lazima nacho kiwe kinapitishwa na bunge/wabunge ili kuweza kuleta usawa wa kivyama.

Ila kwavile anateuliwa na Rais basi lazima atamtumikia Rais.

Ni cheo ambacho huwa kinaendeleza zaidi migogoro badala ya kutatua.

Swali la msingi ni kama bado tunahitaji kuwa na mtu wa kudumu ambaye kazi yake ni usajili na usimamizi wa vyama vya siasa. Mantiki ya kuwa na mtu kama huyu ni nini hasa!?

Mtoa mada somavizuri, ni hivi, Rais Magufuli amteua Bw. Mohammed Ali Ahmed kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar.[ATTACH=full]178036[/ATTACH]

Ingekuwa enzi za JK kwamba mawazo mapya bado yanazalishwa huyu mtu bado angekuwa na kazi.
Ila sasa kwa mtu ambaye hapendi hata fikra mpya huyu mtu hana kazi yoyote licha ya cheo chake kuwa kama mlezi wa vyama vya siasa lakini naona bado kwa wakati huu hana mana.

Hiyo dhana yenyewe kwamba vyama vya siasa vinahitaji Mlezi ni ya kijinga kupindukia!

Kuna nchi niliona vyama vya Siasa vinasajiliwa Mahakama Kuu, hii ni nzuri.
Mgogoro ikitokea Mahakama ndio msuluhishi.

Hapa kwetu nadhani hayo yote yameletwa Kisiasa tu.

Bavicha hata kusoma barua na kuielewa hawawezi wako kama wale wenzao waliopeleka porojo bungeni badala ya mbadala wa bajeti

Ujinga ninaouona mimi ni eti kuwa na mtu analipwa mshahara kusubiri kusajili vyama vya siasa na “kulea” vyama hivyo. Kwanza neno “kulea” linamaanisha utoto, jee hivyo vyama havikui tu mpaka viwe vinalelewa kila siku!?

Uporojo wa ile bajeti ni nini? Hivi huoni aibu kuwa ukimbizini kulikosababishwa na ujinga wa kupenda kusifiwa wa watu wenu?

Umerudi wewe mgonjwa wa stroke?

Hizo porojo kwanini mliziogopa zisisomwe sasa?

Sasa kwa akili ya kawaida tu utaachaje porojo zisomwe Mahali panapohitaji umakini kama Bungeni; huko ni kuwakosea wananchi

Porojo lakini mnakataa zisomwe maana ni porojo ambazo haiziwezi kuathiri bajeti yenu hewa,

Are you insane??

Unaachaje porojo zisomwe Mahali kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania??

Tatizo la Viongozi wenu la uoga halijaanza leo wala jana.

Endeleeni na bajeti yenu hewa kwa kukumbatia maovu yenu

Nilivyosikia kwenye taarifa ya habari ni Naibu Msajili wa vyama vya siasa kwa upande wa Zanzibar na siyo Msajili wa vyama vya siasa Tanzania