Upinzani & CCM wote namba tunazisoma

https://www.youtube.com/watch?v=dK9ZPQjCMbI

Kweli unakuta mashetani ya CCM yamekuja na huku wakati yanashangilia udikiteita wa Jiwe. Nilitegeme nisione jitu lolote la Lumumba huku uhamishoni.

Sana tuu…

Cc: @Mahondaw

Ila wanaona sana aibu ni CCM maana hawakutarajia aisee.

Kwani sisiem nao wanaisoma namba…??

Tuliambiwa huko kwenu mijadala kwenye hilo jukwaa ilikuwa ni kati ya Lumumba na Ufipa, na ilikuwa mikali sana hadi kupelekea jukwaa kufungwa. Sasa kama Ufipa wamekimbilia huku mijadala itaendaje kama Lumumba hasipowafuata huku? Angalizo tu kwamba huku uhamishoni ambako mmekuwa wanakijiji (villagers) muwe wastaarabu, isije mkafungiwa na huku.

Umedanganywa, nani kasema kulikuwa na timu ya Lumumba na Ufipa? Hata ni transit, final destination ni Ulaya au USA… may be South Africa

Tupo uhamishoni,id nyingine

Jf ilikuwa na majukwaa mengi hususani jukwaa la mapenzi, la vichekesho na utani, la historia, la siasa nk. Kati ya majukwaa yote hayo ni jukwaa la siasa peke yake ndilo lililopelekea kufungwa kwa Jf kwani lilikuwa uwanja wa mpira baina ya serikali/ccm (lumumba) vs ukawa/cdm (ufipa). Huko kwenye majukwaa ya mapenzi, utani, vichekesho, sheria, katiba, tiba, historia nk mambo yalikuwa safi sana bila mikwaruzano ye yote, na ilikuwa ni burudani na elimu ya kutosha. Kushindwa kulidhibiti jukwaa hilo la siasa ndicho kimepelekea wamiliki wa Jf wapate heka heka hizo.

Asikudanganye mtu, kule hakukua na wanaccm wala wana ufipa. Bali kulikuwa na wakosoaji na watetezi wa serekali bila kujali itikadi zaidi. Miaka miwili ya mwanzo serekali imejaribu kujenga ushawishi na kutangaza miradi michache ili kunyamazisha wanaohoji, lakini ukosoaji umekuwa mkubwa, uchumi unadondoka kwa kasi, na sasa kumeibuka kashfa ya 1.5 na sauti za kuhoji zimeanza kusikika. Wakati huohuo kuna nyaraka za viongozi wa dini na sehemu zenye mijadala mikali na huru ni mitandaoni tu. Hivyo hakuna jinsi zaidi ya zile sheria ovu kuanza kufanya kazi. Matokeo yake ndio tuko huku uhamishoni.

Hakuna anayetukanwa zaidi ya kupewa ukweli mchungu. Huku unabebwa na hoja zako na sio matusi. Huko nyumbani baada ya mitandao huru kama hii kufungwa acha watu walishwe ujinga wa mwenge na vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serekali.

Hapana Serikali inasomeshwa namba na wakosoaji mpka inahangaika kuziba midomo watu kwa gharama yeyote ile.

Mapambano yanaendelea…

Yatapita

Kulidhibiti kwa vipi? Yaandikwe yale wanayopenda watawala? Rubbish!

V

Kweli salt, yatapita! Na jiwe atapita na pace maker!

mkuu mm kilA cku nayapa vidonge yalikenyulia meno udikteta,sahivi yameleta pumbu zao huku kenyatalk hayana hata aibu

Hayana hata aibu.

https://www.youtube.com/watch?v=DtnjMLyOO9M

Hii haistahili kuita Serikali ni genge la wahuni tu na mafisadi.

Duniani kote vyombo vya habari vyote vikiwemo hivyo vya ki electronic vinaendeshwa kwa kufuata sheria na kanuni za nchi husika. Wala Tanzania si nchi ya kwanza kuwa na sheria kama hiyo. Tena kuna nchi zina sheria kali kuliko hiyo ya Tanzania. Hata hapa uhamishoni wana sheria kama hiyo. Nchi haiwezi kutawalika kama vyombo hivyo vya habari vikaachiwa bila udhibiti wa kisheria. Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka hapa duniani na hata huko mbinguni. Lucifer, aliyekuwa malaika mkuu huko mbinguni, alivuka mipaka ya uhuru wake na akaadhibiwa kwa kutupwa huku duniani akiwa shetani mkuu.