Upimaji samaki kwa rula Bungeni wazua taharuki!

Jana asubuhi watumishi wa wizara ya uvuvi waliingia kwenye mgahawa wa Bunge bila kupata kibali toka kwa Katibu wa Binge, wala Spika wa Bunge, wala Naibu Spika na kuanza kupima samaki kwa “rula” ambao walikuwa wameshapikwa na tayari kuliwa!

Hivi sasa ndiyo Bunge nalo lijionee namna baadhi ya watumishi wa Umma namna wanavyotumia madaraka yao vibaya wakifuata nyayo za kule juu kwa Jiwe!

Vile vile kwa kuwa wizara hiyo inaongozwa na swaiba wake Magufuli, Bwana Mpina, basi tujue kuwa jambo hilo litazimwa kimya kimya…

Naanza kuyakumbuka maneno aliyotamka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wakati ule kuwa utawala wa huyu Jiwe hautamuacha hata mtu mmoja salama…

Ameanza na sisi wapinzani kutunyamazisha na baadaye atakuja kwenu…

Sasa ndiyo hiki kinachotokea kwa watumishi wa wizara ya Uvuvi kujitwalia ujasiri usio wa kawaida na kwenda na “rula” zao na kuanza kuwapima samaki hao!

Hili Taifa, tupende tusipende linaelekea kuangamia, kutokana na kiburi cha mtu mmoja aitwae Magufuli!

Kwa kuwa katika mazingira ya nchi inayofuata utawala bora unaozingatia sheria, kwa kitendo cha hovyo kabisa kilichofanywa na watumishi wa wizara ya Uvuvi, ilibidi barua ya kujiuzulu iwe ishamfikia mteule wake Rais asubuhi hii

Naombeni tafsiri ya neno TAHARUKI

Sio linaelekea, limeshaangamia.

Kama ni loli alilosema limeshapinduka.

Hali ya kutokuwa na Utulivu.

Sasa mbona hujaeleza ni kina nani hao waliokosa utulivu baada ya wapimaji kuingia mgahawani?

Umeuliza maana ya taharuki, nimekujibu hukusema niendelee zaidi ya hapo.

Ungemuuliza mtoa mada labda.

Magufuli hana ubunifu wowote zaidi ya kuua watu wenye maono yaliyomzidi mawaziri wake kama akina mwigulu hata pm hawataweza isaidia nchi .jiwe anategemea maboya kama akina bashite hawezifanikiwa ataondoka madarakani kwa aibu sana muda unazungumza

Hao watu wa Lumumba wana kazi moja tu ya kumtetea Jiwe, hata kama anachokifanya siyo kabisa…

Mkuu achana naye huyo ni kilaza wa Lumumba

Sintofahamu

Inasikitisha sana…

Wabunge kugombania mboga…

Cc: @Mahondaw

umefuata nini huku wewe uvccm? wakati jiwe anaanza kudhibiti mitandao mlikuwa manashangilia, mlidhani nyie mtaruhusiwa hamkujua bila sisi wapinzani nyie mamwezi kupata credit

Propaganda ikitumiwa vibaya inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso…
Mwisho wa kunukuu

Aibu namna hii,mboga kupimwa na ruler kkkkkk
Nalog off

Jambo baya sana kitu kipo tayari kwa kuliwa wewe unakuja mikono yako na mirula sijui ya wapi unaanza kupima sio vizuri kwa afya.
Vip hao samaki waliendelea kutumika au walitupwa

yule boya aliyekua anapima samaki alitegemea igizo lake kushangiliwa na mitandao na vyombo vingine vya habari bila shaka, lakini matokeo yake anaonekana kama taahira tu anayelipwa mshahara wa utumishi bure

!
!
Aisee… Tuko Kwenye Viwanda

Mkienda ferry msisahau rules

Achana nae! Ndio wale wale