Ni utafiti wangu mdogo sana nimeufanya na kugundua ya kwamba kwa siku za karibuni Watazamaji wengi wa Kipindi cha 360 Clouds Tv chenye Watangazaji akina Babie Kabae, Samuel Sasali na Hassan Ngoma wamehama na sasa wanasikiliza sana Kipindi cha Power Breakfast cha Clouds fm chenye Watangazaji akina Babra Hassan, Masoud Kipanya na Ceaser.
Je Uongozi mzima wa Clouds Media Group mmeshaliona hili? Na je mmeshajiuliza ni kwanini hicho Kipindi cha 360 Clouds tv ambacho huko nyuma kilikuwa na mvuto kwa Watazamaji wengi na kilikubalika na Watu mbalimbali siku hizi hali imegeuka mpaka Watazamaji wameanza Kukichoka na kuachana nacho hadi sasa wengine wamekibatiza jina Kipindi cha Wajivuni, Wa Kujipendekeza, Viherehere na Wapenda Sifa?
GENTAMYCINE nina sababu zangu kadhaa za kwanini hali imekuwa hivyo ila naomba Kwanza niwaachie na Wanavijiji / Wakuu wa JamiiForums iliyo ndani ya Kenya Talk nao walipokee hili, walitathmini kisha waanze Kutiririka na Kuserereka nalo kisha nami huko mbele nitakuwa ’ nachombeza ’ moja, mbili tatu.
Ukiona mpaka GENTAMYCINE nimekuja na hii ’ observation ’ yangu hii Kwenu jueni kwamba ’ something is wrong somewhere '. Na hata Kiimani wanasema ukiona Mtu anakusema / anakukosoa jua ya kwamba anakupenda kweli kweli na kukutakia mema na ukiona Mtu anakusifia sana jua kuna 98.9% za kwamba anakusanifu / anakukejeli. Graph ya Kipindi cha 360 Clouds tv kila siku inashuka hivyo amkeni na lifanyieni Kazi hili haraka kama siyo upesi sana ili Kipindi kirudi katika ’ Chati ’ na kuna uwezekano labda kuna ’ Nuksi ’ imeingia au ’ Kirusi ’ kibaya mmekikaribisha na sasa kinawadidimizeni tu bila nyie kujua.
Ila mimi naona ni Yale yale tu maana bado wapo nyumba ile ile kutoka 360 ya Clouds tv kwenda Power Breakfast ya Clouds Fm ni sawa na kutoka chumbani kwenda sebuleni…
Mimi niliacha zamani sana kutazama hicho kipindi
Ingekuwa kwenye football ningewafananisha watangazaji wa 360 na mchezaji anayecheza na jukwaa kutaka sifa [chenga nyingi] matokeo yake anaharibu…
Upande wa pili, PB ilipoteza mvuto baada ya G. Hando na PJ kuondoka lakini usajili wa Kipanya na Siza umekipandisha sana… Kipanya, Barbara na Siza wako vizuri sana, ila PJ wa kawaida tu.
Waswahili mna taabu sana na ni Watu wa ajabu mno! Kila siku mlikuwa mnalalamika aina ya ’ Font ’ ninayotumia na ’ Mwanamume ’ nimesikia ’ Kilio ’ chenu nimeachana nayo badala ya kushukuru mnaanza tena Kuhoji. Namshukuru Mungu siku hizi ’ Matusi ’ yangu yako mbali na Mimi.
Ulishaona wapi mtangazaji wa tv/redio akafungamana na upande mmoja 96percent na akaendelea kupendwa??..kazi kusifia tu,wakati nchi hii ina matatizo laki na upuuzi