Umeijuaje hii kambi ya wakimbizi?

Wakuu heshima kwenu

Ni wazi kuwa sasa tuko ukimbizini kwa muda na tunawashukuru ndugu zetu kwa kutustiri katika hiki kipindi kigumu.

Wengi tulikua tumezoea JF kwa mambo mengi na shida zetu mbali mbali zilitatuliwa kule

Je ,umeijuaje Kenya Talk na hadi ukafika JF ya huku?

Mimi binafsi nilikua nagoogle any kenyan or Ugandan forums ili niweze kuona mada mbali mbali kuhusu world cup,ndio nikajikuta huku.

Wewe umeijuaje?

Yaani sijui nimefikaje huku

Mungu ni mwema wakati wote

nimeletwa na suggestions za google, nadhani kitu kikiwa maarufu kwenye eneo fulani basi uki google kutoka eneo hilo kinakua miongoni mwa majibu ya kwanzakwanza

Kuna chalii etu mmoja fb alitutonya

Mie namshukuru mkuu fulani hivi wa JF ndie aliyenipigia simu.

NimeijuliaTwitter kuna mdau alisema kama umeimiss JamiiForums kuna dawa yake akaweka link kuteleza nazo nmejikuta npo huku Shukran kwake maana nlikua nshaanza kuona mzigo Smartphone

mimi nilikuwa na google sheria za tcra mara ghafla nikaingia kwenye blog moja kuna habari imeandikwa melo akanusha jf kuhamia kenya nikaisoma nikaingia

Mimi nimejaribu tu nikasukumiziwa huku.

Haaaaaaaaaahaaaaaaaa

Kakusukumiza nani huku?
Je ungezama ingekuaje?

Nilimtumia @Demii link kwa simu yake

:D;)

Jamaa yangu alinipa tip via group WhatsApp baada ya kuuliza, wengi wanateseka kwa upweke.Nashauri aliekaribu na Mange amuombe a post link hii.

Nlisikia bbc wakitangaza kuwa Jf imeibukia Kenya…watashindana lakini hawatashinda

Mimi nipo tangu mwaka jana, nilikuwa nasachi mtandao pinzani EAC, ndo nikaona haka kt kanakuna mdogo mdogo kikajiunga

Shukran nilipata

Twitter ndio iliyonileta ukimbizini
Nalog off

Ukigugo jamiiforum hii imekuwa ikiibuka nikajikuta huku…

Aiseee mm nlijjpata huku wakat napitia
News za BBC Swahili nkakuatana na habar
Ya kusema "jamiiforum yakanusha

Mtandao wao kutumika Kenya na kusema haijui chochote kuhusu Jf ya Kenya"

Hapo hapo kukawa na link ya KT
Bhas na mm nkateleza nayo kama
Nashuka mlima kitonga

Utakuwa bila shaka ni member Kennedy wa JF

“Mungu ni mwema wakati wote” huwa anapenda sana kuwrite hayo maneno.