Miti huwa na tuvitu watu hupenda. Kwanza miti ya maembe. Ukiiona tu hivi, wewe na mawe, unairushia. Kanaweza kuwa generous kakuangushie maembe kadhaa ufurahi. Hata miti za popo hurushiwa mawe, na ikiangukia, pengine paipai imebondeka. Hata sielewi mbona popo huwa hivyo. NKT, soft soft tu sana! Niliambia watu wapande miti za paipai polepole na watachuna zile hazijabondeka.
Sasa kuna beshte yangu fulani, mweusi hivi. Jamaa ndio wale Njoki Chege huongelea. Sahii sasa amenunua Subaru ya tatu. Hiyo pia ni ya blue. Hata nashindwa kwani alirogwa! Sasa yeye naye anapenda kugonga miti tu kama watu wengine. Kuna siku nilimpata akigonga ya blue gum akitumia panga nikashangaa sana juu za maembe zilikuwa tu hapo karibu na ilikuwa season yao. Kumuuliza, akasema anataka kujenga nyumba. Right away nikajua tu hiyo nyumba itasimama straight, juu hata vile niliangalia hiyo miti, wacha tu.
Lakini sasa huyu beshte yangu kumbe hakuwa anapenda hiyo mti sana juu hakuiacha ikauke ndio akate bao za roofing, so ni kama hakuwa anafurahia vile ilikuwa imeshikilia roof ya nyumba. Ile Sato ingine vile tulienda ulevini, aliamua kutafuta mti ingine straight kama hiyo ya blue gum, juu hata wewe ukiangalia hizo miti si huwa zimesmama straight? Baaaas, sasa yeye ametoka club hapo K1 akiendesha 189 kph na ni mlevi. Kona ya kwanza, haaaaah. Ya pili tena, haaaa. Vile anaingia tu hivi junction fulani, akaona mti ya stima hapo kando ya barabara. Sijui ni vile ilikuwa imesmama kombo kidogo ni kama ilikuwa imegongwa na Subaru ingine, lakini jamaa akaigonga paaa. Mti hiyo, chini – ikaanguka.
Jamaa pombe zilikuwa zinamuambia ameangukia matunda ya hiyo mti juu kwanza akifika hapo kwa kona, alikuwa anaona ni kama ni season ya mango juu ya vile hapo juu kwa hiyo mti kulikuwa na tuvitu tuvitu za stima - mabulb. Akadhani ni matunda zimeiva mpaka zinawaka. Wapi, kumbe beshte yetu ndio alikuwa ameangukiwa na mti, paaaaaa. Sasa naskia ati anataka agonge miti za zambarau juu hiyo mti ya stima alidhani ina maembe kumbe ni ya stima ilimpiga shock, thiiiittttiiiiiimaaaa!
Hata wewe pia ukitembea tu hapo kwa barabara uone kamti kamesimama hapo na matunda zinakuangalia ni kama zinataka zirushiwe mawe, kwanza angalia kama ni mti ya maembe ama ni ya stima. Miti za stima hazina fruits kijana. Tembeza kiatu tu.
Na staki maswali pi.