Heche kawaambia madini hayaibiwi kama Stroke unavyofikili madini yanaibiwa kwa mikataba mibovu inayoingiwa na CCM na Serikali yake huku mkizuia bunge live na mitandao kutokuwa na sauti
Hitimisho ni kwamba kamwambie aliyekutuma tumefeli kuzuia teknolojia na bado wanatuanika uozo wetu.
Na kuna wafanyabiashara wanaopenda kukwepa kodi wameficha fedha zao nchi jirani na wanarun biashara zao hapa Nchini kwa kutoa cash nchi jirani ; sasa kama hawajali nchi Yao sijui wanategemea nani aijali.
Awamu hii mtaimba kila ngonjera na hatutajali kwakua ndicho ambacho majority ya watanzania walikitaka na wanakitaka.
Wapinzani walikuwa wanatuimbia nyimbo za kudai Rais mwenye maamuzi na asiye lege lege kama walivyokuwa wanadai; amekuja huyu ananyoosha tu bila kuangalia sura.
Upinzani wamefikia uwezo wao wa mwisho kabisa wa kufikiri na Hiki ndicho wanachoamini kimebaki cha kuwasaidia; Hakuna anayepoteza muda kuhangaika na huu utoto wananchi wanamkubali Rais wao na wanakiamini kama mtu sahihi kuisimamia hii nchi iliyokuwa imetekwa na wachache; Hakuna anayefurahia hili Kati ya wale wanufaika wa mfumo usiokuwa na usawa!!
Maslahi yanapoguswa hata kama maamuzi yaliyopelekea hayo maslahi kuguswa Katika macho ya wengi kuwa ni ya busara; wale ambao maslahi Yao yameguswa lazima waone uamuzi huo kuwa hauna busara; hivyo kuifanya tafsiri ya neno busara kuwa tegemezi ya factors mbali mbali