TUSIKUBALI KUSAMBARATISHWA

Wakimbizi wenzangu habari za asubuhi. Kuna mkimbizi mwenzetu ameitambulisha Bongo Forums,ambayo imeundwa na watu fulani. Kasema hao watu ni wenzetu ambao wapo USA.Wakimbizi wenzangu, chooonde, ninawaomba tuwe na msimamo.Kama tumeamua kuwa hapa basi na tuwe hapa. Tukianza kuhangaika, hatimaye tutasambaratika kabisaaa. Hicho ndicho wakitakacho watesi wetu. Tutakuwa tumemegeka vipande vipande na hatimaye kukosa jukwaa moja la kutuunganisha kama jukwaa letu pendwa JAMIIFORUMS ambalo kwa sasa lipo kifungoni. Amani na iwe kwenu.

“Baki na Mimi!” SMS kutoka kwa my love

Huko nyie mwende tu.

Unaweza kujikuta unaungana na Ben Saanane.

Tumeshaanza kupazoea hapa,hamna haja sana ya kuama…

Nimechungulia kule nikakiona kizee kinajiita mwanakijiji, yaani hapohapo nikafunga hiyo forum maana haka kazee kalishaonyesha dalili za kukubaliana na mpuuzi jiwe kabla jf yetu haijafungwa. Kamwe sikubali kujiunga kule.

Hivi mmiliki ni nani? Nimemuona Mzee mwanakijiji kulee

Hapo kwa huyo mzee ndo pamenitisha maana siku hizi haaminiki

Nahis na msiba anahusika, kwakweli hata mimi siuamini mpaka nimjue mmiliki

Hivi umeziona baadhi ya nyuzi za kule? Yaani karibia nyuzi zoooooote kaanzisha mwanakijiji, hapo tu tayari nahisi joka limetega litukamate. Hata akijitokeza mmiliki akajitangaza bado sina imani na mwanzo wa hiyo forum ghafla kuwa na mwnakijiji ambaye kwa kipindi hiki cha awamu hii amekua mpiga debe mzuri sana wa hawa watawala wa kiimla.

Kuna mtu nimemmisi kweli Jf sijui nitampataje hahaha kidding thanks wakenya mmeonyesha ukubwa kutukaribisha WaTz Jf yetu itarudi tu

Usinogewe ndugu nyumba ya jirani tumejificha tu

Mkuu kama wanatoa huduma nzuri watu lazima waende kule, hawa Wakenya, forum ipo slow pia tumewaomba app sasa wakiendelea kuyaweka sandukuni maombi yetu ndio hivyo

Hata mimi siendi huko. Tutakuwa tukisoma tu lakini comment na post ni huku.

Tz wajifunze kwamba ukimuua Osama mmoja watatokea wakina Osama kwa 100.

Naendelea kusoma comments

Karibu sana ukimbizini.

Asante sana mkuu, ebu ngoja tuone kama mkono wa Mzee Baba utafika hadi huku

Hauwezi kamwe labda kama KT ingekua iko Rwanda lakini huku kwa baba wa demokrasia jiwe litaishia kuota jinundu tu

Ni kweli wandugu ni kweli hiyo Bongo forums ifanyiwe uchunguzi isiwe imeundwa kwa njia za hila

Mkuu @Waso wanasema wasiwasi ndio akili, hii forum mwenye imenipa wasiwasi wa kuanza wa kuanza kutoa details zangu baada ya kuwaona baadhi ya lumumba.

Isije ikawa imeanzishwa kwa malengo maalumu.

Hapahapa pananitosha, kuweni makini sana huko.

Hauwezi kamwe labda kama KT ingekua iko Rwanda lakini huku kwa baba wa demokrasia jiwe litaishia kuota jinundu tu