Tuna uhakika gani kama Jamii Forum hii mpya ni Salama?

Awali ya yote nitoe pole kwa wanajamii forum wote kwa kadhia iliyotukuta kule nyumbani,hakika ilikuwa ni hard time kuishi bila JF…thanks God tumekutana huku Ukimbizini tukiwa tumehifadhiwa kwa muda.

Back to topic,baada ya kuenea taarifa ya kuwa JF imehamia Kenya,Max amekanusha vikali kwamba jambo hilo sio la kweli,kutokana na hali hiyo najiuliza hii JF mpya ina usalama gani? sio janja ya TISS wameaunda JF fake ili kuweza kutudukua kiurahisi maana wanajua kabisa asilimia kubwa watakaokuja huku watatumia ID zao zilezile…
Tuwekane sawa kwa hili Wakimbizi wenzangu.

Mkuu unasemaje hii ni JF Mpya?

Huoni kuwa ni subforum ndani ya forum ya KenyaTalk?

Naiita Mpya kwa mantiki kwamba tumeanza upya process zote kujisajiri hadi sred zote ni mpya japo majukwaa ni yale yale,ukiangalia jukwaa mama la siasa kuna nyuzi kama 35 :oops: bila shaka umenielewa mkuu…

This is KenyaTalk.

This is kenyatalk Broadcasting all the way from kiambu. We gonna take a short commercial break then we gonna be right back. Stick around.

Kijana nadhani sisi tuliokuka KT tunapaswa Ku trust the process in a child like faith kila kitu k itakuwa sawa after a while. And hopefully we are safe and tidy. @The Tweet

I’m enjoying!

Wasiwasi wa nini? Mbona Kenya Talks ipo siku nyingi na watu tulikuwa tunavisit huku kitambo tu…

Hilo nalo neno

haina upya wowote, binafsi nilijiunga tangu september 2017

Jf imeamia huku kivipi,server zimeamishiwa uku au??..kama wangekuwa na uwezo huo hao tiss,wangeshafanikisha hilo unalolisema wakati JF ikiwa hewani…huku tupo kwenye forum ya watu…full stop

Tulia pitia comments zote utaelewa logic ya kusema ni mpya…

Sawa…

Am glad nimepata access. Nilikuwa nimeimiss JF nikawa bored sana

Hakuna watu smart hivo kule ndani wa kuplan haya mambo kwa huu muda nina imani niko salama 200%

labda we ndo uwe ao tiss

Akili za wabongo bado saaana, hasa kwenye Technology

Yani mtu mmoja akitoa mawazo yake ya hivyo ndo conclude Bongo nzima??

Utakua na tatizo mahali hii ni Kenyatalk ni forum kama zilizo forum zingine eg Nairaland walicho kifanya hawa jirani zetu ni kutufungulia subforum ya Jamii Forum ambayo ina majukwaa kama ile yenyew na hili halina uhusiano na Jf maana Max alisha kanusha hili suala

Poa tu, at least tuna sehemu ya kutoa "frustrations" zetu…

Afadhali tumepata pa kupumulia

Mkuu tanzania kiteknolojia bado saaaaaana, sio tu kwa mtu mmoja ni Bongo nzima.