Sisi watanzania nchi yetu ni kama shamba tunalolimiliki sisi sote, lakini CCM ni kama mfano wa nyani wala mahindi. Kwa mizaha yetu tumewaachia CCM kwa miaka mingi sana kucheza na nchi yetu huku baadhi ya wenzetu wakiamini iko siku CCM watabadilika ivo kuendelea kuwashabikia.
Kila siku kuna dalili kwamba CCM kuendelea kuwepo madarakani ni zahama kwa nchi yetu. Tatizo letu eti watoa mawazo kwamba wapizani hawajawa na sifa ya kuongoza Tanzania ni hao hao CCM na sisi tunawaamini. Hali ya sasa ni dibaji tu ya kitabu chenye kurasa nyingi sana zenye simulizi za mateso kinachoandikwa hivi sasa na CCM na bila ya shaka watoto na wajukuu zetu watakuja kukisoma!
Wewe madhila yanayoletwa na CCM umeona la JF peke yake?
Kwanza tuliambiwa msikiti mkubwa ni wa Dodoma, sasa umejengwa wa Dar na ndiyo mkubwa kuliko yote. Wa Dodoma ulijenga na Libya na huu wa Dar umejengwa na CCM?
nipo naangalia itv hapa huko madangwa lindi wanalalamika barabara mbovu serikali imewatenga, nikimwangalia mlalamikaji juu kavaa kofia ya ccm ikiwa na picha ya jiwa halaf na t-shirt ya ccm, kwa ufup yupo full green. Nikatafakari nimekosa jb, nimewaacha waendelee kuangalia wakimaliza napanda juu ya bati nafungua dish naenda kuuza hapo karb na kwa majuma ndara moja