Tuko bussy kuangalia mapungufu ya wenzetu tu, wema hatuuoni.

“Naomba kila mtu asogeze kiti mbali na mwenzake, sitaki watu wasogeleane na nikiona mtu anadanganya kwa namna yeyote, huo ndo utakuwa mwisho wa semister yako”,
wote walimjua vema huyu profesa, na walijua kabisa hatanii, wote walittii na darasa lilikuwa kimya kabisaa, tayari wakisubiri kupewa karatasi za mtihani, mtihani wa saikologia.

“Mtu asigeuze hizo karatasi mpaka nitakapo waambia”

Profesa aligawa mtihani na aligeuza upande wa maandishi ulikuwa umefunikwa.

Kisha akawaambia geuzeni na anzeni kufanya, mtihani huu ni wa nusu saa tu.

Sauti za karatasi zilisikika kote, wanafunzi wakifunua kuangalia maswali…

Ghafla wote walikumbwa na mshangao, na waliuwa wakiangaliana na walishangaa kilichokuwepo kwenye karatasi

Karatasi zote zilifanana, zilikuwa nyeupee na kati kati palikuwa na alama kidogo nyeusi.

Profesa akasema, naomba kila mmoja aelezee anachokiona kwenye katasi ya mtihani, fafanua kwa jinsi unavyoweza kuelewa, na mkimaliza naomba karatasi hapa nitasahihisha hapa hapa.

Baada ya muda profesa alikuwa na karatasi za kila mmoja na baada ya kuzipitia zote akasimama na kuanza kuongea.

“Nimepitia mitihani hii, cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja aliyepata, wote mmefeli kabisa”

Maneno haya yaliwaacha hoi wana funzi, huku wakitaka kusikia zaidi,

"Karatasi za mtihani nilizowapa zote zilikuwa nyeupe na kati kati kulikuwa na Alama nyeusi, na nikiangalia hapa, naona mmeeleza vema sana kuhusu hili doa jeusi, wengine wamesema linaigawa karatsi pande nne, wengine wakasema ni mfano wa jua, na MAELEZO YOTE YAMEKUWA YAKIFAFANUA KUHUSU HII ALAMA NYEUSI.

Hii ni vema sana lakini SIJAONA HATA MMOJA ALIYEELEZEA KUHUSU SEHEMU NYEUPE ILOBAKI KWENYE HII KARATASI, KIMSINGI SEHEMU NYEUPE NDIO KUBWA KULIKO NYEUSI , LAKINI KWANINI HAKUNA ALIYEEELEZEA SEHEMU HIYO?"

Profesa, akasema ,sitaweka maksi hizi kwenye kumbukumbu ila nilikuwa nataka kuwafundisha jambo…

HIVI NDIVYO BINADAMU TULIVYO, KATI YA MAMBO MEMA MENGI ALIYONAYO MTU, SISI WENGI HATUYAONI HAYO, AKILI NA MAWAZO YETU YOTE YAKO KWENYE DOA TU, KWENYE KASORO TU, KWENYE MAPUNGUFU TU. MBONA HAKUNA ALISEMA KUHUSU SEHEMU NYEUPE?

TUKO BUSSY KUANGALIA MAPUNGUFU YA WENZETU TU, WEMA WOTE HATUUONI.

TAZAMA UGOMVI ULONAO NA MKE WAKO, MUME WAKO, RAFIKI YAKO, MFANYAKAZI MWENZAKO, MZAZI WAKO

SABABU KUBWA NI MAKOSA ALOFANYA. LAKINI NI KWELI KWAMBA HANA WEMA ALOUFANYA?

HANA UPANDE MZURI? NI KWELI MAPUNGUFU NI MENGI KULIKO MAZURI YAKE?
MAFANIKIO NA FURAHA KATIKA MAISHA YETU YANAANZA PALE TU TUTAKAPOKUWA BUSSY KUELEZEA SEHEMU NYEUPE YA KARATASI NA SIO NYEUSI…

TUNAUMIA NA KULIA KILA SIKU KWAMBA MUNGU HATUJALI, JIULIZE, NI KWELI KATIKA MAISHA YAKO HAKUNA MAMBO MEMA MENGI NA MAKUBWA YA KUYASHUKURU BADALA YA MAPUNGUFU TU?

GEUZA MACHO, TAZAMA SEHEMU NYEUPE… ANZA KUWA BUSSY KUELEZEA MEMA KATIKA KILA KITU KINACHOKUZUNGUKA…

UTASHANGAAAA KWAMBA HUO NDIO ULIKUWA UKUTA UNAKUZUIA USISOGEE

Wanasema baya moja huwa linafunika mazuri yote.

Daah!! Nimeipenda hii

Mkuu umenena sana ila pande zote lazima zizungumziwe

Profesa kama yule ni mwehu. Alikuwa anafundisha kozi gani kwanza ? Lete mtihani unaopima kitu ulichonifundisha

Huyo Prof atakuwa ni mwendawazimu, kwa kawaida karatasi ni nyeupe. Kitu tofauti ndani ya hiyo karatasi ilikuwa ni hiyo alama nyeusi. Huoni bila hata kugeuza hiyo karatasi tayari ilikuwa ni nyeupe? Acheni mifano ya kijinga ili kuhalalisha upuuzi jamani. Maprofessor wa hivyo ndio hao mabingwa nadharia lakini ukiwaleta kwenye uhalisia hata kile wanachofundisha wanashindwa kukifanya kwa mafanikio. Mfano unakuta prof wa uchumi hawezi hata kufungua kibanda cha mpesa, lakini ukimkuta darasani anashangaa kwanini watu wanashindwa kuwa matajiri.

Labda alikuwa Proffesa Maji marefu

Atakuwa Prof. Buguruni

Ukiona unasakamwa sana kwa maneno, ujue karatasi yako inakidoti kidogo cheupe katikati, sehemu yote iliyobakia ni nyeusi…

Cc: @Mahondaw