TUJIFUNZE: SIMULIZI YA JANUARY MAKAMBA

Anasimulia nduguJanuary Makamba

Huyu ndugu anaitwa Profesa Mohamed Janabi, ni bosi kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pale Muhimbili. Ni rafiki yangu wa siku nyingi.

Leo nimeongea naye kwa simu nikakumbuka kisa fulani.
Profesa Janabi alikuwa Daktari Binafsi wa Rais Kikwete wakati nikiwa Msaidizi wa Rais. Miaka kadhaa iliyopita, tulikuwa katika ziara ya Rais Kikwete Mkoa wa Lindi.

Tukiwa kwenye msafara kutoka Nachingwea kwenda Liwale, katikati ya pori, msafara ukapata ajali ndogo. Gari iliyoongoza msafara ilipunguza mwendo ghafla kuepuka kitu na kulazimisha magari yote kwenye msafara kufunga breki ya ghafla.

Nyuma ya gari ya Rais, kulikuwa na gari ya walinzi, halafu kuna gari ya spare ya Rais, halafu gari nyingine kadhaa kabla ya gari ya wazi (pick-up) ya askari wa FFU waliokuwa wamesimama, baadhi wakiwa wameshika mabomba. Baada ya magari yote kupiga break, hii pickup ya FFU ikachelewa kupiga break, ikagonga gari mojawapo kwa nguvu. Bomba za nyuma kwenye pickup zikakunjika, askari kadhaa wakapata majeraha madogo, na mmoja akabanwa na bomba kwenye shingo.

Watu wengi tukakimbilia kwenye ile pick-up kusaidia. Kuna daktari mmoja kutoka Lindi aliyekuwa kwenye ambulance ya msafara akapanda pick-up akamcheki yule askari, akawa hana pumzi na dalili zote zikaonyesha amefariki.

Basi yule daktari akatangaza kwamba yule askari amefariki. Huzuni ikatutanda sote. Ikawa inatafutwa gari kubeba maiti.
Profesa Janabi akapanda ile pickup akaanza kumcheki tena yule askari aliyesemekana amekufa. Mimi nilikuwa nimesimama pembeni. Akaniita nipande pick-up na bwana mmoja anaitwa Juma Kengele, fundi mitambo wa PA sytem ya Ikulu. Akiniambia nimshike yule askari miguu, akaanza kukanda kifua chake na kumpuliza mdomoni (CPR).

Rais akaja karibu na pick-up kushuhudia. Profesa akaendelea na hii kazi huku jasho linamtoka nami nikiwa nimeshika miguu. Baada ya muda kuna mtu akabaini kwamba kwenye ile pick-up kuna mabomu ya mkononi yaliyofunikwa na turubai na ile kazi tulikuwa tunaifanya juu ya mabomu. Tukashuka chini haraka.

Profesa akaendelea. Baada ya dakika 20 nyingine yule askari akazinduka. Baada ya nusu saa akawa anasimamama na kuongea. Profesa Janabi ni shujaa. Kutokata tamaa kumeokoa maisha ya mtu.

The unsung heroes, they go extra mile unnoticed!. And if noticed, we rarely tell them while they are still living to give them extra morale to do More heroic Acts! .

Congrats Prof Janabi keep up the heroic Acts you do EVERYDAY!

Okay…

Mpaka hapo nina wasiwasi kuna watu tunawafukia wakiwa wazima hasa wale wanaogongwa na nyoka maana na mimi nina kisa changu.

Mkuu ebu tupe hicho kisa ili tujifunze zaidi hapa

Vipi walitaka kukubadilisha jina nini mkuu?

Sio mimi mkuu, nilishuhudia Marehemu ambaye alikufa kwa Kung’atwa na nyoka akitokwa na Jasho jambo ambalo lilileta
mtafaruku mkubwa wa ndugu, wengine wakitaka tusubiri siku moja zaidi ili achunguzwe wengine wakipinga hilo
hatimaye akafgukiwa hivyohivyo.

Fanya kushare basi tujifunze!

Tayari hapo Juu, mkuu wewe niyule ambaye tumewahi kukutana India?

Inawezekana Mkuu! India kubwa ile!

Duh…

FISIEM ni FISIEM tu

Daah wangemzika hivi hivi… Halafu huyo dr ndo yupo kwnye msafara wa rais, tatizo likitokea kwa rais si anatangaza hata rais kafa

Umenikumbusha Tutty wangu nlisoma nae Morogoro, way back.

Hahaa sio mimi lakini

Km ulisoma Moro, huenda ndio wewe!

Nilisoma Moro

Basi ndio wewe!

Hahaa hapana sio kwamba najikataa, not my real name

acha woga!

Stori nzuri inavutia na kusikitisha pia