Hebu tunga sentensi kwa kiswahili…
Wacha nijaribu :D:D
Masaa mawili yaliyopita, makali ya njaa yalinilemea sana, nilijihisi mnyonge na nguvu iliniishia, nilikata kauli kwenda jikoni angalau nisife njaa. Nilipofika, nilienda moja kwa moja hadi kwenye jokofu na kuufungua mlango, nikatoa glasi ya sharubati karakara, kisha nikachukua vibanzi nilivyobakisha usiku wa kuamkia leo, kwa kutumia tanuri ya miale, nilipasha vibanzi moto kwa dakika tatu, kisha nikaelekea sebuleni kula. Sasa najihisi mwenye nguvu.
[Kiswahili ni ngumu sana] Ingekuwa ni 17 years ago ningefanya vyema lakini sheng imeadhiri uwezo wangu.
Sikujua kuna walimu wa hii lugha teule miongoni mwetu. Pokea alama zote 40/40. Ni dhana potovu tu kwa wakenya, hususan wasomi kutoka magharibi mwa nchi kuashiria kuwa hati kiswahili ni kigumu, na ndiyo lugha maalum ya mawasiliano, huku takriban asilimia tisini wakiitumia nchini. Shida ya wakenya ni kudharau na kutaka kuonyesha uhodari na ukwasi wa lugha ya kigeni, yaani kiingereza bila kutambua kuwa Kiswahili ndiyo lugha yetu.
Ningekuwa mmoja wa hawa wanariadha ningeongea tu kiswahili, au lugha ya mama waandalizi wakikosa mkalimani shauri yao.