the way wasee huibiwa nairobi is outright alarming manze. so kuna huyu msee anafanyanga job tao kwa movie shop anaitwanga alvo. alvo jana alikuwa ameishia kumeet na joni. alikuwa ashikiwe nyama na machupa kadhaa wakicheki UEFA. nilichapia alvo tusonge na yeye ivo akadinda nikasema ni sawa.
alvo alifika joint flani inakuanga along thika road akapata joni akipiga story na msee flani hapo. akawajoin wakipiga story wakichapa chupa za guiness wakikula nyama. alvo aka assume huyo msee anabonga na joni ni beshte yake. joni akaskia kumwagika akashow alvo wacha afike ivo urinal amwagike alafu atarudi.
huyo msee alikuwa na joni akashow alvo
“brathe niaje si uniokolee na tenje yako nivutie msee flani yangu kuna venye imekatika nare”
alvo kukuwa msee mpoa akamdunga. huyo msee akajitoa nje juu hiyo place ilikuwa na kelele. vile alitoka ivo ndo alienda alafu joni akarudi. huyo msee aliacha beer yake hadi nyama. after kitu dakika 8 ivi alvo akaanza kuingia kibaridi hivi kiasi akauliza joni
“msee beshte yako ameenda wapi”
“beshte mgani huyo”
“si huyo msee ulikuwa na yeye hapa”
“huyo msee hata simjui nilimpata hapa tukaanza kupiga na yeye story”