Waheshimiwa Wabunge
Salaam
Napenda kuwajulisha kuwa Katika kikao Chake Maalum kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 05/11/2025 Kamati Kuu ya Halimashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na mambo mengine imewateua Wanachama wafuatao hapa chini kugombea nafasi ya Spika pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Nafasi ya Spika
- Dkt Tulia Ackson
- Ndg Mussa Azzan Zungu
- Stephen Julius Masele
Nafasi ya Naibu wa Spika
- Ndugu Timotheo Paul Mzava
- Ndugu Daniel Baran Sillo
- Ndugu Najma Murtaza Giga
- Ndugu Mgeni Hassan Juma
Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia ibara ya 105(7) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Mei 2025. Aidha kwa kuzingatia Kanuni ya 10(11) (ii)Fungu la Tatu la Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola Toleo la Machi 2025
Aidha Ratiba Kamili ya Tukio la Upigaji Kura itatangazwa punde taratibu zikikamilika hata hivyo Wabunge Wateule Wote tunatakiwa kuwa Dodoma Jumamosi 8/11/2025
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Waheshimiwa Wabunge