TGO NA TANGAZO LA TV LA KIBAGUZI NA UNYANYAPAA

Kupata watoto ni majaliwa ya Muumba.Tgo wanakera sana na tangazo lao la TV “… watajuaje we we kidume kweli” Wahusika masoko badilisheni,mnakera na kusonesha wengi.

Wametengeneza kutokana na mentality ya jamii ilivyojijengea kuwa kupata mtoto ndio uanaume(ukidume)

weka apa hilo Tangazo wengine hatuangaliagi tv

Pole sana

Mtu mwenye video ya hilo tangazo alipost

Siku zingine ukianzisha ’ Uzi ’ uwe Kwanza Wewe kama Wewe unauelewa ndipo unatuletea Watu wenye ’ akili ’ nyingi hadi tumezichoka tukuelewe tafadhali sawa? Unaweza ukawa una ’ Hoja ’ nzuri / kuntu kabisa ila uwasilishaji wake ukiwa wa Kipopoma / Kipumbavu / Kihovyohovyo utakuwa umeharibu kila Kitu.

Si

Sifa ya tangazo la TV,mbali ya ujumbe wa kuvutia kibiashara,lapaswa kuwa na moral values, lisiwe la kunyanyapaa hata kundi dogo,huhitaji elimu kubwa sana kuelewa madhara kwa kundi hata la wachache kwa tangazo husika Tgo…“.baada kupata mtoto… watajuaje Mie kidume kweli”

Kwani lazima kulitizama?tupa kule

Aisee!

Tangazo linawekwa katikati ya taarifa ya habari utaacha kuliangalia ?

Matangazo mengi ya Tigo huwa yanadhalilisha…

Kweli linakera na kuwachoma wagumba na tasa. Lina tofauti gani na ule wa … @machine ??

Linaonyeshwa TV gani na muda gani ili tulifuatilie maana mmegoma kuliweka hapa

Tatizo lako wewe umeleta hapa kana kwamba kila mtu analifahamu hilo tangazo wakati wengine hata kulijua hatulijui ndio maana lazima ,upate maoni ya aina hiyo bora hata ungeliweka hapa ili hata asiyelijua alijue!!!

Kweli halipo vizuri watu ambao hawajabahatika kupata watoto si ajabu watakuwa wanazima hata redio au tv wakati wa tangazo hili. Liondolewe tafadhali