Tetesi za soka 22 Juni 2018

Borussia Dortmund ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Uhispania na Chelsea Alvaro Morata, lakini klabu hiyo ya Bundesliga inaweza ikashindwa kumsajili kutokana na mahitaji ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anayetaka kitita cha £45m.

Spurs ina matumaini ya kumsajili winger wa Croatia Ante Rebic, 24, huku klabu ya Eintracht Frankfurt ikitaka kumuuza kwa dau la £26.3m.

Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri ameanza kupanga kikosi chake cha ukufunzi katika klabu ya Chelsea licha ya hatma ya mkufunzi Antonio Conte kutotatuliwa.

Lucas Torreira anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Sampdoria kwa dau la £26m, huku Arsenal ikimnyatia kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 22-kutoka Uruguay.

Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, ameshauriwa kujiunga na klabu ya ligi ya Marekani DC United na aliyekuwa mchezaji mwenza Steven Gerrard.

Kiungo wa kati wa Sevilla na Argentina Ever Banega, 29, anataka hakikisho kutoka kwa mkufunzi wa Arsenal Unai Emery kabla ya kukubali kujiunga na klabu hiyo.

Beki wa Uturuki na Freiburg Caglar Soyuncu, 22, anataka kujiunga na Arsenal.

Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 30, anasema kuwa anapenda kujifurahisha na tayari amezungumza na wachezaji wenzake katika kikosi cha Ubelgiji nchini China na ligi ya Marekani MLS.

Klabu ya Fenerbahce imeanzisha mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25 Marco van Ginkel.

45 m from 70m, sait …

China na America Ndio hununua water tu, sababu ya experiences au!?

Yaani wazee tu!

Nani hutazama hizo ligi za Marekani na Uchina? Mchezaji akiwa bado ananawiri kimchezo lazima awe kwenye ligi maarufu, au atasahaulika na kawaida, umaarufu ndio unaoleta kitita kikubwa kwa mchezaji…
Ndiposa Uchina na MLS ndipo retirees huenda kumalizia kabumbu yao; na unatoka na bonge la mihela…