Tetesi:Nape Nnauye Kutimkia Upinzani Muda Wowote, Vikao Vya Siri Baina Yake Na Zitto, Mbowe Vyanaswa

Breaking News: MBUNGE WA MTAMA KWA TIKETI YA CCM NAPE MOSES NNAUYE KUHAMIA UPINZANI MUDA WOWOTE.

-Afanya kikao cha siri na viongozi wa upinzani

  • Viongozi hao wamsaka kwa udi na uvumba
  • Mwenyewe atoa masharti mazito

Tarehe 27/05/2018 Mbunge huyo, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-WAZALENDO, Zitto Kabwe na Mbunge wa Hai, Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe walifanya kikao cha siri katika Hoteli ya MEDITERRANEO iliyopo Kawe jijini DSM kuhusiana na Nape kuhamia Upinzani (picha hapo chini). Nape alitoa sharti la kukutana na Zitto na Mbowe kwa pamoja baada ya viongozi hao wa upinzani kwa wakati tofauti kumpigia simu kila mmoja akitaka ahamie kwenye chama chake.

Kikao hicho kilifikia makubaliano ya kuwa ACT-WAZALENDO waungane na CHADEMA kabla ya NAPE hajatangaza kuhamia upinzani. Tamko la Zitto na Mbowe kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu 31/05/2018 wakati wa mazishi ya Marehemu Samson Kasuku Bilago ni utekelezaji wa awali wa masharti ya Nape.

Tarehe 12/06/2018, Nape alipata wakati mgumu kutoka kwa watu wanaoaminika ni wana CCM wenzake lakini mara zote alikingiwa kifua na watu wanaodhaniwa ni wapinzani wakiongozwa na Zitto (tweets hapo chini) pale alipoweka bandiko kwenye akaunti yake ya Twitter lenye maneno: “Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao… kimya kimya!”, akionekana kulaani Agizo la TCRA kuwataka wamiliki wa Mitandao ya kijamii na blogu ambao hawajafanya usajili kusitisha huduma zao. Mtandao wa Jamii Forums ni kati ya ile iliyoshindwa kutekeleza masharti ya TCRA hadi sasa. Nape alishambuliwa kwa vile akiwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, alisimamia kupitishwa kwa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016. Wapinzani wake kwenye mjadala huo wanaona kama hatua ya TCRA ni mwendelezo wa utekelezaji wa alichokiasisi NAPE.

Kuhamia upinzani kwa NAPE MOSES NNAUYE kutahitimisha safari ya wale wote waliowahi kumshambulia aliyekuwa Waziri Mkuu na aliyejiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND, EDWARD LOWASSA kumfuata huko CHADEMA. (Wahenga wanasema: Usimtukane mamba kabla haujavuka mto).

Wengine waliowahi kumshambulia Lowassa kwa ufisadi na Kauli zao kwenye mabano, ni pamoja na: PETER MSIGWA (Anayemshabikia Lowassa akapimwe akili); YERICKO NYERERE(Wakati Magufuli na Mwakyembe wanahangaika kuwaletea wananchi maendeleo, kuna Paka Shume linazunguka Makanisani na Misikitini kusaka kura); GODBLESS LEMA (Ni heshima kwa Mungu kumzomea na kumtukana mwizi na fisadi); TUNDU LISSU (CCM wameruhusu fisadi kuchukua fomu ya kugombea urais - ni hatari); FREDERICK TLUWAY SUMAYE (CCM wakimruhusu Fisadi kugombea urais nitachukua maamuzi magumu); FREEMAN MBOWE (Wananchi wanachoma moto vibaka wanamuacha LOWASSA anakula bata mitaani).

[ATTACH=full]175640[/ATTACH]
[ATTACH=full]175641[/ATTACH]
[ATTACH=full]175642[/ATTACH]

Siasa Choo Hizi!

Hahaha Hatafanikiwa huyo
anaruka mkojo na Kukanyaga kinyesi
Ngoja aende ili tumjue vizuri na kupambana nae Kisawa sawa
upande wangu naona kama huyu ni Zigo ndani ya Ccm na Kirusi ndani ya mwili wa Ccm
Nenda Nape tena hata leo

Lumumba kwa kukimbia vivuli vyao hawajambo.

Nape huyu huyu aikimbie CCM au CCM ndiyo imkimbize?

The last kick of the dying horse hatofika kokote after all saivi he’s like no body zile siasa alizozizoea is no longer exist, pole yake though najua huu ni umbea

Posho bado buku 7 au mmeongezewa?

nape bado hayuko sawa, bao la mkono lamtesa

… dhambi haijawahi kumuacha mtu salama!.. akazane kutubu!

Nape hawezi kuhama CCM,
Ni Muoga yule,
Alishasema ye ndio atakua wa mwisho kutoka CCM

Udaku

Dhambi ya bao la mkono inamtesa amechangia tupate raisi wa ajabu ajabu

Hakuna namna kwasasa ahamie tu upinzani,maana hata kwa ccm hafit tena

Anajizika kisiasa

Hizi ni ngonjera za watu wa CCM coz huyu jamaa amekuwa na maoni tofauti na wao so wanataka kumvua au kumtoa chamani kiani kama msaliti.

Natamani sana kuona upinzani kama ule wa 2010 pamoja na siasa zake…Ni kazi sana kufanya siasa za mitandaoni.

Ni vijana wa Lumumba wanazusha tu!!!

Kwahiyo akihamia upinzani Jf ndo itarejea, kwanza huyo mpuuzi ndo alichangia sana kutorushwa kwa bunge live
Hii ni Toilet paper ambayo bado inatumiwa na CCM pindi wakishamiliza kuharisha.

Hana ujasiri wa kutoka CCM huyo ni boya tu sana sana kinachomsumbua ni kutemeshwa uwaziri.

Hmm!..