TATIZO NYOTA.
1.Auliziwa Fulani,angali mume wa mtu
Naachwa Mimi jamani,naonekana si kitu
Ama nyota ngu angani,tayari yashika kutu
Nahisi tatizo nyota,ndo mana siuliziwi.
2.Japokuwa mi kapela,hata namba kaninyima
Jana nilitoka hola,rafiki nilimtuma
Nikamuhonga vidola,na mate akanitema
Nahisi tatizo nyota, ndo mana siuliziwi.
3.Nikatunga vishairi,labda atanielewa
Nikapanga kimahiri,vina bila kuchelewa
Binti yule mashuhuri,mi nje nkatolewa
Nahisi tatizo nyota,ndo maana siuliziwi.
4.Nyota’li jisafishia,nkaenda kwa Waganga
Eti’li kujipatia,kwanza nijifanye mwanga
Mwenzenu nkahofia,kukamatwa nikiwanga
Nahisi tatizo nyota,ndo mana siuliziwi.
5.Au nitumie nguvu,labda ntaja mpata
Nimmteke kimabavu,kwa nguvu zile za kwata ?
Ama nitumie nyavu,shida sitaki kujuta
Nahisi tatizo nyota,ndo mana siuliziwi.
6.Akilini anitesa,nawaza kuuza shamba
Sijui apenda pesa,maneno yangu ni pamba
Kwa lipi nitamnasa,ama mi bado mshamba ?
Nahisi tatizo nyota,ndo mana siuliziwi.
SHAIRI-TATIZO NYOTA
MTUNZI-Idd Ninga, Tengeru Arusha.
+255624010160
[email protected]