Kwa kuwa umemzungumzia Ronaldo kwa kudhani labda nilimaanisha ya kuwa namkubali Ronaldo sivyo ilivyo
Lakini nikwambie hesabu ubora wa wachezaji wa ureno kisha hesabu ubora wa wachezaji wa Argentina kisha watoe hao key players wao(messi na Ronaldo)wabadalishane mataifa uone kama world kapu haiendi Argentina kwa Ronaldo na mess wa ureno hata hatua ya makundi hatofika.
Chukua mess na barca nje ya la liga namaanisha Uefa huwa anasaidia vipi timu yake chukulia tu kuanzia miaka ile ingali kijana kabisa hadi hivi karibun amesaidia nini ndani ya klabu yake?! Kama vyenga hata Okocha alipiga vyenga vingi tu lakini anamchango gani?!
Chukulia timu za bara Amerika kisha ziweke na Bara ulaya uone wapi mpira upo kisha chukua timu ya ureno iweke katikati yao utaona ni nani anastahili kuitwa mchezaji
Mchezaji haimaniishi upige vyenga,magoli mengi Hapana mchezaji lazima uyafanye yote hayo na kisha uwe na uhamashishaji kwa wengine wajue wanacheza na mtu uliewazidi kila kitu.
Nadhani ukitazama utaona Madrid haikufaa kuchukua Uefa msimu huu mana walikuwa na kiwango kibovu lakini wachezaji wakahamasishana na kocha pia mwisho wa siku wakacheza kwa kujituma wakachukua kombe.
Messi ni mzuri sana lakini wenzie wamekuwa wakimlalamikia kwa kuwa na maamuzi kama kocha,akikuchukia basi hutacheza,mkikwaruzana kidogo hutacheza,yupo uwanjani na vijana wadogo wanaotafuta jina lake Kama kina Dybala piga ua watacheza kujitafutia wao ili waoneshe na wao wanaweza bila yeye ambae anamaamuzi juu yao wote,hana mbinu za uhamasishaji kwa wenzie hayupo kama nahodha wa timu…
Mbali na yote ni mwaka huu tu ndio kamzidi Ronaldo kwa kuingiza pesa nyingi na ni kwa sababu Ronaldo hajasaini mkataba mpya,ronaldo anakampuni nyingi za matangazo kuliko mess so ndo utajua yupi ni bora kati yao.
Lakini mimi ukiniuliza mchezaji gani bora kwangu,sitamtaja Mess wala Ronaldo nitakutajia INIESTA na Marcelo miaka yote kwa uchezaji wao mzuri uliotukuka na ukitizama hawa ndo wanafanya Ronaldo awepo na Mess awepo
Marcelo anacheza kisha akifika mbele anajitahid amtafute Ronaldo alipo ili ampe mpira
Iniesta akicheza anamtafuta Messi alipo na mara chache alikuwa anamtafuta Suarez ambae anajua jukumu lake ni kumpa Messi tu ili amalizie.
Sishabiki yeyote kati yao wala sikutaka unitajie Ronald ndani ya uzi huu ambao naamini mtoa mada alikuwa hataki kuzungumzia Ronaldo maana ukitazama ureno inaweza kutolewa na irani na Argentina ikasonga kam itampiga Nigeria so bado mambo mabichi acheni ushabiki maandazi zungumzeni soka
Huwezi kusema ipo nyuma ya Brazil na Uruguay wakati wenzao wapo mbele ya ufaransa na ujerumani na wamenyanyua kwapa na kombe la ulaya.
Assit moja na goli nne wakati mwingine anazaidi ya vyote
Marcelo na Iniesta bado wapo juu ya hao wote mtazamo wangu lakini sijalazaimisha iwe kwa wote.
Ronaldo anamwaka huu tu wa kucheza mpira mzuri na mess anamwaka mmoja mbele wa kucheza mpira 31y-33y