Kama mlivyoona kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari tarehe 26
Novemba 2025, Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limejadili na kupitisha azimio kuhusu
kile walichokiita “Post-election killings and the deteriorating human rights
situation in Tanzania, including the case of imprisoned opposition leader Tundu
Lissu” ambalo pamoja na madai mengine Azimio limetoa wito kwa Kamisheni ya EU
kusubirisha kwa muda utiaji saini wa makubaliano ya Programu ya Ushirikiano baina
ya Tanzania na EU kwa Mwaka 2025 (Annual Action Plan – AAP 2025) yenye thamani
ya Euro milioni 156.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.pdf (1.5 MB)