Tanzania Railways Corporation (TRC) to begin construction of urban electric railways in Dar es Salaam in 2026 - Wakenya wanaumia

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limekamilisha hatua za awali za upembuzi wa mradi wa reli za mijini, na ujenzi unatarajiwa kuanza mwakani ili kuboresha usafiri wa umma Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, amesema shirika hilo limejipanga kuanza hatua ya pili ya mradi huo, sambamba na kuendeleza maboresho ya miundombinu na huduma za reli nchini.

Akiwa katika ziara fupi Stesheni ya Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewahakikishia wananchi kuwa miundombinu ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma iko salama, akisisitiza ulinzi shirikishi kwenye korido zote za reli huku TRC ikisema itaendelea kuhakikisha ubora na usalama unadumishwa katika maeneo yote ya miundombinu yake.

No Brain Yap GIF