Tanzania News: Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka (UDART) inatarajia kupokea mabasi mapya 99 ya BRT phase I - Wakenya wanaumia sana

Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka (UDART) inatarajia kupokea mabasi mapya 99 kama sehemu ya mpango wa kuboresha huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam.

Mabasi haya mapya yanakuja katika wakati ambapo mahitaji ya huduma za UDART yanaendelea kuongezeka, na yanatarajiwa kuongeza ufanisi, upatikanaji na ustahimilivu wa mfumo wa usafiri wa umma.

Kulingana na ratiba ya usafirishaji, awamu ya kwanza ya mabasi hayo itawasili Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 Desemba 2025, huku awamu ya pili ikitarajiwa kufika tarehe 15 Januari 2026. Ujio wa mabasi haya unatarajiwa kuongeza idadi ya safari, kupunguza muda wa kusubiri, na kuboresha huduma kwa maelfu ya wakazi wanaotumia mfumo wa mabasi yaendayo haraka kila siku.

Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuimarisha miundombinu na kutoa huduma bora, salama na ya uhakika kwa wananchi.

Maboresho haya yanatarajiwa kuchangia kupunguza msongamano, kuongeza tija katika shughuli za kila siku za wakazi wa Dar es Salaam, na kuimarisha ustawi wa sekta ya usafiri wa umma.

https://www.instagram.com/p/DRmxij2DAys/