Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 08 Julai, 2018 ameongoza mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL).
SHEREHE ZA BOMBARDIER ZIKIISHA, TUHESABU HASARA ZA ATCL. #Mtatiro J
Naambiwa kuwa tumetumia takribani Dola za Marekani Milioni 63 (Tshs Bilioni 130) ili kuokoa mchakato wa kimahakama wa ndege hii iliyokuwa imezuiwa Canada (Kwa mujibu wa Mhe. ZZK). Bilioni 130!
I mean tumepaswa kuwalipa wadai wetu kila kitu, deni lao walilokuwa wanatudau, riba zake na gharama za kesi (ndiyo wakakubali kuondoa kesi ya madai mahakamani ili tumalizane nje ya mahakama). Kichekesho ni kuwa, gharama halisi za kununua ndege ya Bombardier kama tuloileta ni Dola Milioni 31 tu (Tshs Bilioni 63).
Halafu wapo watu wanataka tushangilie eti serikali imenunua ndege. Yani wapo watu wao wanataka tu kuona ndege inapaa, hawataki kujua hasara tuliyopata ambayo haizibiki (maana Bombardier mbili za awali zimeshatuletea hasara ya Tshs Bilioni 223 kwa miaka miwili tu).
Kwa wanaopiga hesabu, kama Bombardier ya tatu (hii ya sasa) kwenye kuileta peke yake tumeshaingia hasara ya Bilioni 67, ukiongeza na hasara ya Shs Takribani Bilioni 195 ambazo tutazipata kwa mwaka huu wa fedha kwa kusimamia uendeshaji wa Bombardier zote tatu (hasara ya Tshs Bilioni 65 kwa Bombardier Moja x 3 kwa mwaka huu unaoendelea), unaelewa wapi tutakakoekekea.
I mean in 3 years, tutakuwa tumepoteza Tshs Bilioni 223 + Tshs Bilioni 67 + Tshs Bilioni 195 = Hasara ya Takribani Tshs Bilioni 485 (Nusu Trilioni).
Mnajua kwa nini nayasema haya, nchi moja moja zilizojaribu kuendesha mashirika ya ndege kwa pesa za serikali, nchi hizo zilishindwa vibaya. Air Rwanda ambayo inamilikiwa na serikali ya Rwanda kwa asilimia 99, kila mwaka inapata hasara kubwa. Wamejaribu kuiuza bila mafanikio wamekosa wateja wenye hela ambazo serikali inazitaka.
Hivi sasa tuzungumzapo, AIR INDIA iko sokoni, inauzwa baada ya serikali ya India na utajiri wake wote kujaribu kuiendesha bila mafanikio. I mean uendeshaji wa mashirika ya ndege ni jambo mtambuka na lenye mchakato uliokokotolewa vilivyo. Uendeshaji wa shirika la ndege hauihitaji ndoto za mtu mmoja tu, kwamba “…nchi yangu haina ndege wacha nizinunue.”
Yes, unaweza kununua madege 10 au 20, na kila dege linakupa hasara ya Bilioni 100 kwa mwaka, kwa hiyo madege 20 yakakupa hasara ya Shs Trilioni 2 kwa mwaka (Milioni Elfu Moja x 20), wananchi wakawa wanashangilia kuwa sasa tunazo ndege 20, lakini kwa mwaka mmoja madege hayo peke yake yanakula Trilioni Mbili (bajeti nzima ya kuendesha serikali ya Tanzania mwaka wa fedha wa 2000/2001).
Jambo lingine, uzoefu wa umiliki wa madege ni kiwa huwa hayanunuliwi kwa pesa taslimu. Madege huchukuliwa viwandani serikali inakuwa mdhamini kisha shirika la ndege linaanza kuilipia ndege husika huku ikifanya kazi. Hiyo ndiyo nidhamu ya ununuzi wa ndege duniani kote.
Afrika ni bara la ajabu sana, huko nyuma sote tulilalamika juu ya namna Shirika letu la ndege ATCL lilivyokufa, tukasema shirika hili linapaswa kufufuliwa, basi ufufuaji wa shirika letu ungelipitia kwenye michakato ya kitaalamu na yenye tija zaidi kuliko kudhani kuwa kununua madege kwa hasara kubwa na kuziendesha kwa hasara kubwa ndiyo hasa matamanio ya watanzania.
Watanzania wangelipenda kuwa na shirika la ndege litakaloongozwa kwa mustakabali mwema, siyo mbwembwe, sifa, na hasara. Ndiyo maana, miaka michache baadaye tusishangae kusikia kuwa nchi ilipoteza matrilioni ya fedha kuifufua ATCL ambayo imeendelea kuwa mzigo kwa taifa.
Wapo watu wanaumia sana tukizungumza mambo haya, wanasema kazi yetu ni kupinga, tukiwaeleza kwa takwimu kuwa elimu yetu inakufa wanasema hatuna shukrani, ni kama vile hiyo elimu inayotolewa ni hisani na si wajibu wa serikali. Tukisema uchumi wa nchi ni mbovu na unaanguka wanasema tumetumwa na wazungu, tunaionea Tanzania wivu, kana kwamba sisi ni wageni hapa Tanzania.
Naomba muitunze POST hii, baada ya miaka mitano tutaelezana ATCL iko wapi, nina uhakika asilimia 100 kuwa tumeingilia mguu wa kushoto kwenye kuifufua ATCL na andiko hili litakuwa rejea lakini sasa hivi kwa sababu tunamshangilia mfalme kwa vinubi na filimbi, tuendelee kusheherekea.
Siku sherehe zikiisha tutasaidiana kupiga hesabu ya hasara za ATCL vs VIPAUMBELE VYA WATANZANIA na huo ndiyo wakati tutazungumza lugha moja, maana kila tulizungumzalo NINYI hulitambua baada ya miaka mitano au kumi. Mnaelewa polepole mno. #Mtatiro J
Usiwadharau Wa TZ.Watatupita tukiendelea na mchezo wetu.Waibii wa pesa za NYS,NCPB na wakuleta sukari mbovu wangekuwa wa TZ Magufuli angekuwa ashawatia ndani
Sio madharau, wakiendelea ni bora zaidi maana itakuwa changamoto kwetu, Lakini propaganda haileti maendeleo. Mtu akisema progress ipo 50% isiwe propaganda tuu, maana itakuwa ni kelele tuuu…
Hahahahaha!! Kutoka kwenye chumba cha mama yangu!!!?
Boy do you know the meaning of PPP and Economic Inclusion?
This is the attachment read for your own benefit