Tanzania: IDARA YA MAMBO YA KALE; MAFANIKIO YA IDARA KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 - 2019

[CENTER]DIBAJI [/CENTER]
Malikale ni urithi wa matokeo ya maisha ya binadamu katika harakati za kukabiliana na mazingira anayoishi wakati wa kutekeleza shughuli za kila siku. Katika kumudu maisha ya kila siku binadamu au kiumbe chochote lazima awe mbunifu wa teknolojia mbalimbali zitakazomwezesha kutengeneza vitu au rasilimali zitakazomwezesha kuishi na wale wanaoshindwa hutoweka. Malikale hizi zinazotengenezwa na jamii husika baada ya kuonekana ni muhimu huzitunza na kuzihifadhi na hatimaye hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine miaka hadi miaka. Urithishanaji huu wa malikale unakuwa ni sehemu ya utamaduni wao na huheshimiwa na jamii husika. Hivyo, Jamii huweka taratibu, kanuni na sheria za kuwezesha raslimali hizo kulindwa, kuhifadhiwa na hurithishwa kwa utaratibu maalum. Vilevile Malikale hujumuisha masalia ya binadamu, wanyama na mimea ambayo kutokana na tafiti mbalimbali zimeonyesha na kudhihirisha historia ya mabadiliko ya viumbe hivi kimaumbile, kifikra, kiteknolojia na kisayansi. Malikale pia hujumuisha mazingira aliyoishi au yaliyotumika na binadamu, wanyama na mimea.

Soma zaidi:
http://www.maliasili.go.tz/uploads/Mafanikio_ktk_Idara_ya_Mambo_ya_Kale.pdf