TANZANIA,CHINA KUSHIRIKIANA KUONGEZA WATALII

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

TANZANIA na China zimeamua kushirikiana kwa lengo la kukuza soko la utalii nchini.

Hivyo imeelezwa watu maarufu na mashuhuri wa nchi ya China akiwamo mwigizaji maarufu wa nchi hiyo Maododo atakuwa miongoni mwa watakaokuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.Hatua inakuja kipindi ambacho kumekuwa na uchache wa watalii wa kutoka China kuja Tanzania,hivyo moja ya mkakati wa kuongeza watalii hao ni kuweka ushirikiano kwenye eneo la utalii.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) uliofanyika leo Dar es salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema uhusiano wa China na Tanzania ni wa muhimu sana.

Amefafanua kuwa wana wanampango wa kubadilisha mfumo ili Wachina waingie kwa wingi nchini na kuboresha soko la utalii nchini China.Amesema fursa ya Wachina kushirikiana katika utalii i ni nzuri hasa ikitumika ipasavyo.

"Kwani wamepata nafasi ya kuwatumia watu maarufu kutoka nchini China ili kusaidia kutangaza utalii wa Tanzania na moja ya watu maarufu watakaotumika kama mabalozi wa kutangaza Utalii ni muigizaji maarufu kutoka China.
[B][I]
https://1.bp.blogspot.com/-K6uTm6-gvZ0/WnnEnB_Xk2I/AAAAAAACKoI/GDwiNPOWBgoyKfotQo3NC7-VkNYXNvfbwCLcBGAs/s640/01.JPG
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya Utalii jijini Dar es Salaam.
[B][I]
https://2.bp.blogspot.com/-sao6YkghMag/WnnEnOSID-I/AAAAAAACKoE/Vhv3CwYjcHQvXe_AiWFrbCWJSuC8DiodgCLcBGAs/s640/02.JPG
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Miyayo akizungumza kuhusiana na utalii nchini wakati wa mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya Utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

https://3.bp.blogspot.com/-NxkXu9L7xEE/WnnEnKmxMPI/AAAAAAACKoM/-53TI8toAMkDEOfEmrDgeE_5uACq_6IkACLcBGAs/s640/03.JPG
Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori na Mtafiti wa Sokwe Mtu Sokwe wa Mkoa wa Kigoma ,Dk. Jane Goodal akizungumza kuhusiana na Utalii nchini leo jijini Dar es Salaam.

https://3.bp.blogspot.com/-vpDkqdq4Iuo/WnnEoH-JIeI/AAAAAAACKoU/odZLDLcfrBYrwRY2RDjZT0acMAerMQXagCLcBGAs/s640/05.JPG
Msanii Maarufu nchini China, Nanping Liu akikabidhi zawadi Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori na Mtafiti wa Sokwe Mtu Sokwe wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Jane Goodal katika Mkutano wa Utalii jijini Dar es Salaam.
[/I][/B][/I][/B]

there you go with your chinese masters again…

Pass our greetings to your massa